63-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfunulia Wahyi Kwa Aina Zaidi Ya Moja
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
63-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfunulia Wahyi Kwa Aina Zaidi Ya Moja
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٥١﴾
Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi, au Hutuma Mjumbe, kisha Anamfunulia Wahy Ayatakayo kwa idhini Yake; hakika Yeye ni Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Mwenye hikmah wa yote. [Ash-Shuwraa: 51]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pekee ambaye Wahyi wake kutoka kwa Allaah (عز وجل) ulikuwa ni wa aina kadhaa miongoni mwazo ni aina zifuatazo:
Aina Ya Kwanza Na Ya Pili: -Kama kwa sauti ya kengele, au kupitia Jibriyl (عليه السلام) kwa umbile la mtu:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ ـ رضى الله عنهاأَنَّ الْحَارِثَ بْنَ هِشَامٍ ـ رضى الله عنه سَأَلَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ كَيْفَ يَأْتِيكَ الْوَحْىُ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَحْيَانًا يَأْتِينِي مِثْلَ صَلْصَلَةِ الْجَرَسِ ـ وَهُوَ أَشَدُّهُ عَلَىَّ ـ فَيُفْصَمُ عَنِّي وَقَدْ وَعَيْتُ عَنْهُ مَا قَالَ، وَأَحْيَانًا يَتَمَثَّلُ لِيَ الْمَلَكُ رَجُلاً فَيُكَلِّمُنِي فَأَعِي مَا يَقُولُ " قَالَتْ عَائِشَةُ رضى الله عنها وَلَقَدْ رَأَيْتُهُ يَنْزِلُ عَلَيْهِ الْوَحْىُ فِي الْيَوْمِ الشَّدِيدِ الْبَرْدِ، فَيَفْصِمُ عَنْهُ وَإِنَّ جَبِينَهُ لَيَتَفَصَّدُ عَرَقًا.
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها) Al-Haarith bin Hishaam alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) “Ee Rasuli wa Allah! Wahyi unakujia vipi?” Rasuli wa Allaah akajibu: “Wakati fulani unanijia kama sauti ya kengele, aina hii ya Wahyi ni ngumu zaidi kwangu kuliko zote na kisha hali hiyo hunipitia baada ya kuwa nimeshafahamu kile nilichofunuliwa. Wakati mwingine Malaika huja katika umbile la mtu, hunizungumzisha na kuzingatia anayosema.” ‘Aaishah amesema: Kwa hakika nilimwona (Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم) akiletewa Wahyi siku ya baridi kali na akaona jasho likimdondoka usoni (baada ya kumalizika Wahyi). [Al-Bukhaariy]
Aina Ya Tatu: Allaah (عز وجل) kumsemesha moja kwa moja nyuma ya pazia mfano vile alipoongea naye pindi Alipompandisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mpaka mbingu ya saba katika safari ya muujiza ya Al-Israa Wal-Mi’raaj akamfaridhisha na Ummah wake Swalaah tano.
Pia kama ilivyoelezewa katika Hadiyth ifuatayo:
عنْ أَبِي قِلاَبَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَتَانِي اللَّيْلَةَ رَبِّي تَبَارَكَ وَتَعَالَى فِي أَحْسَنِ صُورَةٍ قَالَ أَحْسَبُهُ قَالَ فِي الْمَنَامِ فَقَالَ يَا مُحَمَّدُ هَلْ تَدْرِي فِيمَ يَخْتَصِمُ الْمَلأُ الأَعْلَى قَالَ قُلْتُ لاَ . قَالَ فَوَضَعَ يَدَهُ بَيْنَ كَتِفَىَّ حَتَّى وَجَدْتُ بَرْدَهَا بَيْنَ ثَدْيَىَّ أَوْ قَالَ فِي نَحْرِي فَعَلِمْتُ مَا فِي السَّمَوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ قَالَ يَا مُحَمَّدُ هَلْ تَدْرِي فِيمَ يَخْتَصِمُ الْمَلأُ الأَعْلَى قُلْتُ نَعَمْ . قَالَ فِي الْكَفَّارَاتِ . وَالْكَفَّارَاتُ الْمُكْثُ فِي الْمَسَاجِدِ بَعْدَ الصَّلَوَاتِ وَالْمَشْىُ عَلَى الأَقْدَامِ إِلَى الْجَمَاعَاتِ وَإِسْبَاغُ الْوُضُوءِ فِي الْمَكَارِهِ وَمَنْ فَعَلَ ذَلِكَ عَاشَ بِخَيْرٍ وَمَاتَ بِخَيْرٍ وَكَانَ مِنْ خَطِيئَتِهِ كَيَوْمَ وَلَدَتْهُ أُمُّهُ وَقَالَ يَا مُحَمَّدُ إِذَا صَلَّيْتَ فَقُلِ اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَتَرْكَ الْمُنْكَرَاتِ وَحُبَّ الْمَسَاكِينِ وَإِذَا أَرَدْتَ بِعِبَادِكَ فِتْنَةً فَاقْبِضْنِي إِلَيْكَ غَيْرَ مَفْتُونٍ قَالَ وَالدَّرَجَاتُ إِفْشَاءُ السَّلاَمِ وَإِطْعَامُ الطَّعَامِ وَالصَّلاَةُ بِاللَّيْلِ وَالنَّاسُ نِيَامٌ " .
Kutoka kwa Abu Qilaabah kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Alinijia Rabb wangu (تبارك وتعالى) usiku mmoja kwa Sura nzuri kabisa.” (Mmoja wa msimuliaji) alisema: Nadhani alisema ilikuwa katika ndoto. “Kisha Akasema: Ee Muhammad! Je, unajua kundi lilotukuka kabisa linajishughulisha na nini?” Akasema: “Nikasema hapana! Akaweka Mkono Wake baina ya mabega yangu hadi nikahisi kupoza kwa kwake kwa ubaridi kati ya kifua changu.” Au alisema: “Kwenye koo langu. Kwa hivyo nilijua yaliyomo mbinguni na yaliyomo duniani. Akasema: Ee Muhammad! Je, unajua kundi lilotukuka kabisa linajishughulisha na nini? Nikasema: Naam, katika Mukaffaraat (‘amali zinazofuta madhambi) na ‘amali zinazofuta madhambi ni kukaa Msikitini baada ya Swalaah na kutembea kwa miguu kuelekea Swalaah za Jamaa na Isbaagh Al-Wudhwuu (kutawadha kikamilifu pamoja na kuwepo uzito na ugumu), na atakayefanya hivyo ataishi kwa kheri na atakufa kwa kheri, madhambi yake yatakuwa kama siku aliyomzaa mama yake (hana madhambi). Akasema (pia): Ee Muhammad, utakaposwali sema:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ، وَتَرْكَ الْمُنْكَرَاتِ، وَحُبَّ الْمَسَاكِينِ وَإِذَا أَرَدْتَ بِعِبَادِكَ فِتْنَةَ فَاقْبِضْنِي إِلَيْكَ غَيْرَ مَفْتُونٍ
Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kufanya mema yote, kuacha munkari zote, na kuwapenda masikini, na Unapotaka kuwatia waja wako majaribuni (fitnah), basi Nifishe mimi bila kujaribiwa.
Akasema: Na kupandishwa daraja ni kueneza Salaam na kulisha chakula na Swalaah za usiku watu wanpokuwa wamelala.” [At-Tirmidhiy]
Aina Ya Nne: Ndoto Ya Kweli
عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنَّهَا قَالَتْ أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنَ الْوَحْىِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلاَّ جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الْخَلاَءُ
Amesimulia ‘Aaishah (Mama wa Waumini): (رضي الله عنها): Wahyi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ulianza kwa ndoto njema usingizini na alikuwa haoni ndoto isipokuwa ni kweli kama ulivyo mwanga wa mchana, na alipendezeshwa kujitenga. [Al-Bukhaariy]
Aina Ya Tano: Kumjia Jibriyl (عليه السلام) kwa umbo lake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ﴿٢٣﴾
Na kwa yakini alimuona (Jibriyl) katika upeo wa macho ulio bayana. [At-Takwiyr: 23]
Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ ﴿١٣﴾ عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ ﴿١٤﴾ عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ ﴿١٥﴾
Na kwa yakini amemuona (Jibriyl) katika uteremko mwingine. Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa. Karibu yake kuna Jannah ya Al-Ma-waa. [An-Najm: 13 – 15]
Na kuhusu Kuali hizo za Allaah (سبحانه وتعالى), Aaishah (رضي الله عنها) alisema katika Hadiyth ndefu:
أَنَا أَوَّلُ هَذِهِ الْأُمَّةِ سَأَلَ عَنْ ذَلِكَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ : إِنَّمَا هُوَ جِبْرِيلُ لَمْ أَرَهُ عَلَى صُورَتِهِ الَّتِي خُلِقَ عَلَيْهَا غَيْرَ هَاتَيْنِ الْمَرَّتَيْنِ رَأَيْتُهُ مُنْهَبِطًا مِنْ السَّمَاءِ سَادًّا عِظَمُ خَلْقِهِ مَا بَيْنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ
Mimi ndiye wa kwanza wa Ummah huyu ambaye alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hilo (kumuona Jibriyl), akasema: “Hakika yeye ni Jibriyl. Sijawahi kumwona katika umbo lake la asili ambalo aliumbwa nalo isipokuwa kwa nyakati hizo mbili (zinazokusudiwa katika Aayah hizo); Nilimwona akishuka kutoka mbinguni na kujaza (angani) kutoka mbinguni kuja duniani kwa umbo lake kubwa mno la mwili.” [Muslim]