Imaam Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy: Majani Ya Sidri (Kunazi) Ni Tiba Dhidi Ya Uchawi
Majani Ya Sidri (Kunazi) Ni Tiba Dhidi Ya Uchawi
Imaam Al-Haafidwh Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy (Rahimahu Allaah)
Amesema Al-Hafidhw bin Hajar (Rahimahu Allaah): (Mtu) Achukue majani saba ya Sidri (Kunazi) (yaliyo) mabichi kisha ayatwange kati ya mawe mawili, kisha ayachanganye na maji na (kisha) ayasomee Ayatul-Kursiyy na Al-Qawaaqil: (Suwrah Al-Jinn, Al-Kaafiruwn, Al-Ikhlaasw, Al-Falaq, An-Naas) kisha avivie (apulizie) mara tatu na kisha ayaoge, basi, itamuondoshea yote yaliyomsibu. Na ni nzuri pia kwa yule aliyezuiwa (ashindwaye kumuingilia) Ahli yake kwa uchawi." [Fat-hul Baariy (10/233)]
Al-Qawaaqil ni Suwrah zinazoanzia na قُلْ nazo ni:
Al-Jinn (72), Al-Kaafiruwn (109), Al-Ikhlaasw (112), Al-Falaq (113), An-Naas (114)
Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi kuhusu Ruqya ya Sihri:
10-Ruqya: Kutafuta Shifaa: Poza Ya Maradhi, Sihri (Uchawi) Katika Baadhi Ya Vyakula