Sharh (Maelezo) Ya Masharti Ya لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّه
Sharh (Maelezo) Ya Masharti Ya لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّه
Mawqi’ Dorar.com
Imetarjumiwa Na Alhidaaya.com
Sharti Ya Kwanza: ‘Ilmu (Elimu, Maarifa, Ujuzi, Utambuzi)
Makusudio yake ni kuitambua kwa maana yake inayokusudiwa kwa kukanusha na kuthibitisha, ambavyo vinaondosha ujinga, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ
Basi jua kwamba: laa ilaaha illa-Allaah (hapana muabudiwa wa haki ila Allaah) [Muhammad (47: 19)]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٨٦﴾
Na wala wale wanaowaomba badala Yake hawana uwezo wa kumiliki uombezi isipokuwa yule aliyeshuhudia kwa haki nao wanajua. [Az-Zukhruf: 86]
Anakusudia: Wameshuhudia kwa
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّه
ilhali wanajuwa kwa nyoyo zao maana ya kile walichokitamka kwa ndimi zao. Amesema tena Allaah (سبحانه وتعالى):
شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾
Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye; na (pia) Malaika na wenye elimu (kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan (3: 18)]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾
Sema: Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua? Hakika wanakumbuka wenye akili tu. [Az-Zumar: 9]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ
Hakika wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni ‘Ulamaa… [Faatwir: 28]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ ﴿٤٣﴾
Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu. Lakini hawaifahamu isipokuwa wenye elimu. [Al-‘Ankabuwt: 43]
Na katika Hadiyth Swahiyh:
عَنْ عُثْمَانَ بِنْ عَفَّان رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Uthmaan bin ‘Afaan (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayefariki akiwa anajua kwamba:
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ
laa ilaaha illa Allaah – hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah
ataingia Jannah)). [Muslim]
Sharti Ya Pili: Yaqini:
Yaqini inayoondosha shaka, nayo ni kuwa yule mzungumzaji ni mwenye yaqini juu ya maana inayojulishwa na neno hilo kwani Iymaan pekee haiwezi kusaidia kama anaeamini hana yaqini, sasa itakuwaje kama hiyo yaqini ikaingiwa na shaka?
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ﴿١٥﴾
Hakika Waumini ni wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake, kisha wakawa si wenye shaka, na wakafanya jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Allaah. Hao ndio wakweli. [Al-Hujuraat: 15]
Allaah (سبحانه وتعالى) Ameweka masharti ya mtu kuwa mkweli wa Iymaan kwa Allaah na Rasuli Wake, ni kutokuwa na shaka, na yule mwenye shaka basi huzingatiwa kuwa ni mnafiki, Allaah (سبحانه وتعالى) Atuepushe na wale aliowataja kwenye Kauli Yake:
إِنَّمَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَارْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِي رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ﴿٤٥﴾
Hakika wanaokuomba ruhusa ni wale ambao hawamwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na nyoyo zao zina shaka, basi wao katika shaka zao wanasitasita. [At-Tawbah: 45]
Na katika Hadiyth Swahiyh:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: قَال رسول الله صلى الله عليه وسلم: أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ لاَ يَلْقَى اللَّهَ بِهِمَا عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ فِيهِمَا إِلاَّ دَخَلَ الْجَنَّةَ " . مسلم
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ
Nashuhudia kwamba
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
laa ilaaha illa Allaah na kwamba mimi ni Rasuli wa Allaah
Mja atakayekutana na Allaah bila ya kuwa na shaka yoyote juu ya hii (misingi miwili) ataingia Jannah. [Muslim]
Na katika Riwaayah:
لاَ يَلْقَى اللَّهَ بِهِمَا عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ فَيُحْجَبَ عَنِ الْجَنَّةِ "
Mja atakayekutana na Allaah bila ya kuwa na shaka yoyote juu ya hii (misingi miwili) hatoepushwa kuingia Jannah. [Muslim]
Na pia,
((يَا أَبَا هُرَيْرَةَ (وَأَعْطَانِي نَعْلَيْهِ) قَالَ: اذْهَبْ بِنَعْلَيّ هَاتَينِ فَمَنْ لَقِيتَ مِنْ وَرَاء هَذَا الْحَائِطِ يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّهُ مُسْتَيْقِنا بِهَا قَلُبُهُ فَبَشّرْهُ بِالْجَنّةِ))
((Ee Abaa Hurayrah (akanipa viatu vyake) Nenda na viatu vyangu hivi, utakayemkuta nyuma ya ukuta huu akiwa anakiri moyoni na anashuhudia kwamba:
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki ila Allaah akiwa amethibitika nayo moyoni, mbashirie Jannah)) [Muslim]
Pamewekwa sharti, ili mtamkaji wa
لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّهُ
aingie Jannah moyo wake uwe na yaqini ya hilo Neno na moyo hauna shaka, kwa hiyo sharti ikikosekana basi na kile kilichowekewa sharti hakipatikani (Jannah, Pepo).
Sharti Ya Tatu: Kukubali.
Kukubali kile ambacho kimebebwa na hili Neno la
لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّه
kwa moyo wake na ulimi wake, na Allaah Anatusimulia Allaah (عزَّ وجلّ) khabari za waliopita ambapo ni kuwaokoa waliolikubali na jinsi Allaah Alivyowatesa wale waliopinga na kulikataa, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ﴿٢٣﴾ قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ ۖ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ﴿٢٤﴾ فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿٢٥﴾
Na hivyo ndivyo Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mji mwonyaji yeyote yule isipokuwa wamesema matajiri wake wenye starehe na taanusi: Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini, na hakika sisi ni wenye kufuata nyao zao. (Kila Rasuli) Alisema: Japo kama nimekujieni na uongofu zaidi kuliko ambao mliyowakuta nao baba zenu? Wakasema: Hakika sisi tunayakanusha yale mliyotumwa nayo. Basi Tukawalipizia, kisha tazama vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha. [Az-Zukhruf: 23- 25]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٠٣
Kisha Tunawaokoa Rusuli Wetu na wale walioamini. Hivyo ndivyo haki Kwetu kuwaokoa Waumini. [Yuwnus: 103]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَانتَقَمْنَا مِنَ الَّذِينَ أَجْرَمُوا ۖ وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾
Na kwa yakini Tuliwatuma kabla yako, Rusuli kwa watu wao, wakawajia kwa hoja bayana; basi Tukawalipiza wale ambao wamefanya uhalifu. Na ni haki daima Kwetu kuwanusuru Waumini. [Ar-Ruwm: 47]
Pia vile vile Anatukhabarisha Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyowaahidi Jannah wale wenye kuikubali, na kuwaahidi adhabu kali wale walioipinga, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٢٢﴾ مِن دُونِ اللَّـهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْجَحِيمِ ﴿٢٣﴾ وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ ﴿٢٤﴾ مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ ﴿٢٥﴾ بَلْ هُمُ الْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ ﴿٢٦﴾ وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٧﴾ قَالُوا إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ الْيَمِينِ ﴿٢٨﴾ قَالُوا بَل لَّمْ تَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٢٩﴾ وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ ۖ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَاغِينَ ﴿٣٠﴾ فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَا ۖ إِنَّا لَذَائِقُونَ ﴿٣١﴾ فَأَغْوَيْنَاكُمْ إِنَّا كُنَّا غَاوِينَ ﴿٣٢﴾ فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ ﴿٣٣﴾ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ ﴿٣٤﴾ إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾ وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾
(Malaika wataamrishwa): Wakusanyeni wale waliodhulumu na wenziwao na yale waliyokuwa wakiyaabudu. Badala ya Allaah, basi waongozeni kwenye njia ya moto uwakao vikali mno. Wasimamisheni, hakika wao ni wenye kuulizwa. (Wataulizwa): Mna nini hamnusuriani? Bali wao leo wamesalimu amri. Na watakabiliana wenyewe kwa wenyewe kuulizana. Watasema: Hakika nyinyi mlikuwa mkitujia kutoka kuliani (kutushinda nguvu). Watasema: Bali nyinyi wenyewe hamkuwa wenye kuamini. Na hatukuwa na madaraka juu yenu, bali mlikuwa watu wapindukao mipaka kuasi. Basi ikahakiki juu Yetu kauli ya Rabb wetu; hakika sisi bila shaka ni wenye kuonja (adhabu). Kisha tukakupotoeni hakika sisi tulikuwa wenye kupotoka. Basi hakika wao Siku hiyo katika adhabu ni wenye kushirikiana. Hakika hivyo ndivyo Tuwafanyavyo wakhalifu. Hakika wao walipokuwa wakiambiwa: Laa ilaaha illa Allaah, Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hutakabari. Na wanasema: Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi majnuni?! [Asw-Swaffaat: 22-36]
Akajaalia sababu ya kuwaadhibu ni kupinga kwao kauli
لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّه
na kumkadhibisha yule aliekuja nayo (Nabiy), hawakupinga kilichopingwa na kauli hiyo, na wala hawakuthibitisha kilichothibitishwa na kauli hiyo, bali walisema kwa kupinga na kiburi. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ ﴿٥﴾ وَانطَلَقَ الْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ امْشُوا وَاصْبِرُوا عَلَىٰ آلِهَتِكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ يُرَادُ ﴿٦﴾ مَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي الْمِلَّةِ الْآخِرَةِ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا اخْتِلَاقٌ ﴿٧﴾
Amewafanya waabudiwa kuwa ni Ilaah Mmoja? Hakika hili ni jambo la ajabu mno! Na wakaondoka wakuu miongoni mwao kwamba: Nendeni zenu na subirini juu ya waabudiwa wenu, hakika hili ni jambo linalokusudiwa. Hatukusikia haya katika mila ya mwisho, haya si chochote isipokuwa ni jambo lilozushwa tu. [Swaad: 5 - 7]
Na wakasema tena:
أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾
Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi majnuni?! [Asw-Swaffaat: 36]
Akawakadhibisha Allaah (عز وجل) juu ya maneno yao dhidi ya Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٧﴾
Bali (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) amekuja kwa haki, na amewasadikisha Rusuli (waliotangulia). [Asw-Swaffaat: 37]
Hadi mwisho wa Aayah hizi, kisha Akasema Allaah (سبحانه وتعالى) katika hali ya wale wataoikubali kauli ya
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
Laa Ilaaha Illa Allah:
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٤٠﴾ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ ﴿٤١﴾ فَوَاكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ ﴿٤٢﴾ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٤٣﴾
Isipokuwa waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlasi zao. Hao watapata riziki maalumu. Matunda; nao ni wenye kukirimiwa. Katika Jannaat za neema. [Asw-Swaffaat: 40 – 43]
Mpaka mwisho wa Aayah hizo. Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا وَهُم مِّن فَزَعٍ يَوْمَئِذٍ آمِنُونَ ﴿٨٩﴾ ﴾
Atakayekuja na jema, basi atapata bora zaidi kuliko hilo; nao watakuwa katika amani na mafazaiko ya Siku hiyo. [An-Naml: 89]
Na katika Hadiyth Swahiyh:
عَنْ أَبِي مُوسَى، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَثَلُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ مِنَ الْهُدَى وَالْعِلْمِ كَمَثَلِ الْغَيْثِ الْكَثِيرِ أَصَابَ أَرْضًا، فَكَانَ مِنْهَا نَقِيَّةٌ قَبِلَتِ الْمَاءَ، فَأَنْبَتَتِ الْكَلأَ وَالْعُشْبَ الْكَثِيرَ، وَكَانَتْ مِنْهَا أَجَادِبُ أَمْسَكَتِ الْمَاءَ، فَنَفَعَ اللَّهُ بِهَا النَّاسَ، فَشَرِبُوا وَسَقَوْا وَزَرَعُوا، وَأَصَابَتْ مِنْهَا طَائِفَةً أُخْرَى، إِنَّمَا هِيَ قِيعَانٌ لاَ تُمْسِكُ مَاءً، وَلاَ تُنْبِتُ كَلأً، فَذَلِكَ مَثَلُ مَنْ فَقِهَ فِي دِينِ اللَّهِ وَنَفَعَهُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ، فَعَلِمَ وَعَلَّمَ، وَمَثَلُ مَنْ لَمْ يَرْفَعْ بِذَلِكَ رَأْسًا، وَلَمْ يَقْبَلْ هُدَى اللَّهِ الَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ "
Abuu Muwsaa Al-Ash-‘ariyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mfano wa uongofu na elimu ambayo Allaah Amenituma kufikisha ni kama mvua kubwa inayoanguka juu ya ardhi, baadhi yake (hufikia) katika ardhi yenye rutuba imenyonya maji ya mvua na ikaleta mimea na majani kwa wingi. Na baadhi yake (ardhi) ilikuwa nzito na ikazuia maji ya mvua (kupenya katika ardhi) na Allaah Akawanemeesha watu kutokana nayo na wakaitumia kwa kunywa, kunyweshea wanyama wao na kwa ajili ya umwagiliaji na kilimo kwenye ardhi hiyo. Na baadhi yake ilikuwa si yenye rutuba ambayo haikuweza kukamata maji wala kutoa mimea (hivyo ardhi hiyo haikutoa faida yoyote). (Ardhi) Ya mwanzo ni mfano wa mtu anayetambua Dini ya Allaah na akapata faida (kutoka na elimu) ambayo Allaah Ameishusha kupitia kwangu (Manabii na Wanachuoni) na akaisomesha kwa wengine. (Ardhi) Ya mwisho ni mfano yule ambae hakuinua kichwa chake kwa ajili ya hilo (mwongozo wa Allaah) na wala hakukubali uongofu wa Allaah ambao nimetumwa nayo” [Al-Bukhaariy]
Sharti Ya Nne: Kunyenyekea (Kufuata bila kuacha):
Kunyenyekea kwa kufuata kile kinachojulishwa na Neno
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
Laa Ilaaha Illa Allaah
unyenyekeaji unaopinga kuacha. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ
Na rudini kila mara kutubu kwa Rabb wenu na jisalimisheni Kwake. [Az-Zumar: 54]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ ﴿١٢٥﴾
Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah naye ni mtendaji ihsaan [An-Nisaa: 125]
Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ
Na anayeusalimisha uso wake kwa Allaah, naye akawa ni mtenda ihsaan, basi kwa yakini ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika. [Luqmaan: 22]
Anakusudia kushikamana na
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
Laa Ilaaha Illa Allaah:
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِلَى اللَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٢٢﴾
Na kwa Allaah ni hatima ya mambo yote. [Luqmaan: 22]
Na maana ya
يُسْلِمْ وَجْهَهُ
anayeusalimisha uso wake ni:
anyenyekee, akiwa ni mhisani na mwenye kumpwekesha Allaah. Na asie usalimisha uso wake kwa Allaah na hakuwa mhisani, basi mtu huyo hakushika kishiko chenye nguvu, na hiyo ndio maana ya kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَن كَفَرَ فَلَا يَحْزُنكَ كُفْرُهُ ۚ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ فَنُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٢٣﴾ نُمَتِّعُهُمْ قَلِيلًا ثُمَّ نَضْطَرُّهُمْ إِلَىٰ عَذَابٍ غَلِيظٍ ﴿٢٤﴾
Na anayekufuru, basi isikuhuzunishe kufuru yake. Kwetu ni marejeo yao, Tutawajulisha yale waliyayatenda. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani. Tutawasterehesha kidogo, kisha Tutawasukumiza kwenye adhabu nzito. [Luqmaan: 23 – 24]
Na huu ndio unyenyekevu uliotimia na ndio malengo yake.
Sharti Ya Tano: Ukweli:
Ukweli unaopinga kukadhibisha, nako ni mtu kutamka
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
Laa Ilaaha Illa Allaah
kwa ukweli kutoka moyoni mwake, moyo wake uende sambamba na kile kinachotamkwa na ulimi wake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
الم ﴿١﴾ أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾ وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ﴿٣﴾
Alif Laam Miym. Je, wanadhani watu kwamba wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao ndio wasijaribiwe? Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao, ili Allaah Awatambulishe wale walio wakweli na ili Awatambulishe walio waongo. [Al-‘Ankabuwt: 1 – 3]
Mpaka mwisho wa Aayah hizi, na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu wanafiki ambao wamelitamka neno hilo
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
kwa uongo:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿١٠﴾
Na miongoni mwa watu wako wasemao: Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho hali ya kuwa si wenye kuamini. (Wanadhani) Wanamhadaa Allaah na wale walioamini lakini hawahadai ila nafsi zao na wala hawahisi. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah Akawazidishia maradhi, na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha. [Al-Baqarah: 8 – 10]
Mara nyingi Allaah (سبحانه وتعالى) Amezitaja hali zao akaweka wazi walivyokuwa wakivificha na Akadhihirisha fedheha zao, sehemu si moja ndani ya Qur-aan, kama vile Suwrah Al-Baqarah, Aal-‘Imraan, An-Nisaa, Al-Anfaal, At-Tawbah na Suwrah nzima imekuja ikielezea hali ya wanafiki, na zisizokuwa hizo, na imekuja Hadiyth:
عَنْ أنَس بِن مالِك رضي الله عنه عن النَّبِيّ صلى الله عليه وسلم قال: (( مَا مِنْ أَحَدٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ صِدْقًا مِنْ قَلْبِهِ إِلَّا حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَى النَّارِ))
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakuna mtu atakayekiri na kushuhudia kwa kusadikisha moyoni mwake kwamba:
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ
laa ilaaha illa Allaah – hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba
مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ
Muhammad ni Rasuli wa Allaah, isipokuwa Allaah Atamharamisha na Moto)). [Al-Bukhaariy (128) Muslim (32)]
Imeweka sharti ya kuokoka na moto kwa ataetamka
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ
‘’Laa Ilaaha Illa Allaah‘’
atamke akiwa mkweli kwenye moyo wake, na haitamsaidia ile kutamka tu bila ya kusadikisha moyoni, imekuja tena katika Hadiyth ya Anas bin Maalik na Twalhah bin ‘Ubaydillaah (رضي الله عنهما) katika kisa cha Mbedui ambaye ni Dhwamaam bin Tha’alabh Waafid bin Sa’d Bin Bakr alipomuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Hukmu za Kiislaam akamuuliza:
هَلْ عَلَىَّ غَيْرُهَا؟ قَالَ " لاَ، إِلاَّ أَنْ تَطَّوَّعَ ". فَأَدْبَرَ الرَّجُلُ وَهْوَ يَقُولُ: وَاللَّهِ لاَ أَزِيدُ عَلَى هَذَا وَلاَ أَنْقُصُ. قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَفْلَحَ إِنْ صَدَقَ ".
Je, kuna nyengine mbali na hiyo?” Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم) “Hapana, isipokuwa ukitaka kutoa sadaka.” Mtu huyo akaondoka, huku anasema, “Wa-Allaahi sitazidisha juu ya hayo wala kupunguza.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema, “Atafuzu ikiwa amesema kweli.” [Al-Bukhaariy]
وفي بعض الروايات إِنْ صَدَقَ لَيَدْخُلَنَّ الْجَنَّةَ
Na katika Riwaayah nyenginezo: “Akiwa mkweli, bila shaka ataingia Jannah.”
Sharti pekee ya kufaulu na kuingia Jannah ni kutamka ilihali yu mkweli kwenye moyo wake.
Sharti Ya Sita: Ikhlaasw (kufanya jambo kwa niyya safi kwa ajili ya Allaah Pekee).
Ikhlaasw ni kuyasafisha matendo kwa niyya safi kutokana takataka za ushirikina. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ ۚ وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ
Tanabahi! Ni ya Allaah Pekee Dini iliyotakasika [Az-Zumar:3]
Anasema tena Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ
Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini [Al-Bayyinah: 5]
Anasema tena Allaah (سبحانه وتعالى)
فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ ﴿٢﴾
Basi mwabudu Allaah kwa kumtakasia Dini Yeye. [Az-Zumar: 2]
Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ ﴿١١﴾
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi nimeamrishwa nimwabudu Allaah nikiwa mwenye kumtakasia Dini Yeye. [Az-Zumar: 11]
Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلِ اللَّـهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُ دِينِي ﴿١٤﴾
Sema: Allaah Pekee namwambudu nikimtakasia Yeye tu Dini yangu. [Az-Zumar: 14]
Anasema tena Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا ﴿١٤٥﴾ إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّـهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ۖ
Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto; na wala hutompata kwa ajili yao mwenye kunusuru. Isipokuwa wale waliotubu na wakatengenea na wakashikamana na Allaah na wakakhalisisha Dini yao kwa ajili ya Allaah; basi hao watakuwa pamoja na Waumini. [An-Nisaa: 145 – 146]
Na Aayah nyenginezo kadhaa.
Na katika Hadiyth Swahiyh:
عن أَبِي هُرَيْرَةَ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللهِ مَنْ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ؟ قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلى اللهُ عليهِ وَسَلَّمَ: ((لَقَدْ ظَنَنْتُ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ أَنْ لا يَسْأَلَني عَنْ هذَا الْحَدِيِثِ أَحَدٌ أَوَّلَ مِنْكَ لِما رَأَيْتُ مِنْ حِرْصِكَ عَلَى الْحَدِيثِ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَنْ قَالَ: لا إِلهَ إِلاَّ اللهُ خَالِصَاً مِنْ قَلْبِهِ أَوْ نَفْسِهِ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Nani atakayefurahika kabisa kwa Shafaa’ah (uombezi) wako Siku ya Qiyaamah: Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Nlidhani ee Abaa Hurayrayh kwamba hakuna yeyote asiyekuwa wewe atakayeniuliza maelezo haya kwa vile jinsi nilivyoona himma yako juu ya jambo hili. Atakayefurahika zaidi kati ya watu kwa Shafaa’ah yangu Siku ya Qiyaamah ni atakayesema:
لا إِلهَ إِلاَّ اللهُ
laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah
kwa niyyah safi moyoni mwake au nafsi yake)). [Al-Bukhaariy]
Na pia,
عن عِتْبَانَ بْن مَالِكٍ الْأَنْصارِيَّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ يَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللَّهِ ))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Itbaan bin Maalik Al-Answaariyy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Ameharamisha An-Naar kwa anayesema:
لا إِلهَ إِلاَّ اللهُ
laa ilaaha illa Allaah
akitafuta Wajihi wa Allaah)). [Al-Bukhaariy (425), Muslim (33)]
Na pia,
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، رضى الله عنه قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَا قَالَ عَبْدٌ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ قَطُّ مُخْلِصًا إِلاَّ فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ السَّمَاءِ حَتَّى تُفْضِيَ إِلَى الْعَرْشِ مَا اجْتَنَبَ الْكَبَائِرَ "
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna mja asemaye
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
Kwa ikhlaasw (Niyya safi) isipokuwa itafunguliwa milango ya mbingu mpaka ifikie ‘Arsh, madamu atajiepusha na al-kabaair (madhambi makubwa).” [At-Tirmidhiy]
Sharti Ya Saba: Mapenzi (Kuipenda Laa لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ)
Kuipenda Kalimah hii ya
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
Laa Ilaaha Illa Allaah
kwa maana yake inayojulisha na kwa watu wake wanaoifanyia kazi wanaolazimiana na masharti yake na kubughudhi kila maana inayopingana na Kalimah hiyo, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ
Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. [Al-Baqarah 2: 165].
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ
Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri; wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. [Al-Maaidah: 54]
Ametukhabarisha Allaah (عز وجل) ya kuwa waja wake Waumini wana mapenzi zaidi ya kumpenda Allaah, ni kwa sababu wao hawakushirikisha kwenye mapenzi ya kumpenda Allaah na chochote kile, kama walivyofanya wale waliodai kumpenda Allaah katika washirikina ambao walijifanyia kinyume na Allaah washirika wakawapenda kama wanavyompenda Allaah, na alama ya mja kumpenda Rabb wake ni kuyatanguliza mapenzi ya Allaah kuliko chochote hata kama yanakwenda kinyume na matamanio yake, na kukibughudhi Anachokibughudhi Allaah hata kama yeye anakitamani. Na kuwapenda Anaowapenda Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuwachukia Anaowachukia Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), na kumfuata Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kufuata athari zake na kukubali mwongozo wake; haya yote ni katika alama za mapenzi na ndio masharti pekee, ambapo mtu hawezi kusema anapenda bila kukamilika haya masharti, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلًا ﴿٤٣﴾
Je, umemuona yule aliyefanya hawaa yake kuwa ndio mwabudiwa wake? Je, basi utaweza wewe kuwa ni mdhamini wake? [Al-Furqaan: 43]
Anasema tena Allaah (سبحانه وتعالى):
أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّـهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِن بَعْدِ اللَّـهِ ۚ
Je, umemuona yule aliyejichukulia hawaa zake kuwa ndio mwabudiwa wake, na Allaah Akampotoa juu ya kuwa na elimu na Akapiga mhuri juu ya masikio yake na moyo wake; na Akaweka kifuniko juu ya macho yake? Basi nani atamuongoa baada ya Allaah? [Al-Jaathiyah: 23]
Kila mwenye kuabudu pamoja na Allaah kitu kingine, huyo kwa uhakika atakuwa anaabudia matamanio ya nafsi yake, bali kila mja anapomuasi Allaah basi sababu yake inakuwa ni kuyatanguliza matamanio yake kabla ya amri za Allaah, na makatazo Yake, Anasema Allaah kuhusiana na kupenda na kuchukia:
قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَءَآؤُاْ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ
Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni, na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha ya kudumu milele mpaka mumuamini Allaah Pekee. [Al-Mumtahinah: 4]
Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ
Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda wanaompinga Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allaah) Amewaandikia katika nyoyo zao iymaan. [Al-Mujaadala: 22]
Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ
Enyi walioamini! Msifanye Mayahudi na Manaswara marafiki wandani. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani; basi hakika yeye ni miongoni mwao. [Al-Maaidah: 51]
Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾ قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٢٤
Enyi walioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu marafiki wandani ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya iymaan. Na yeyote miongoni mwenu atakayewafanya marafiki wandani basi hao ndio madhalimu. Sema: Ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake (au waume) zenu na jamaa zenu na mali mliyoichuma na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake, na majumba mnayoridhika nayo, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Rasuli Wake na kufanya jihaad katika njia Yake; basi ngojeeni mpaka Allaah Alete Amri Yake (ya adhabu). Na Allaah Haongoi watu mafasiki. [At-Tawbah: 23 – 24]
Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ
Enyi walioamini! Msifanye adui Wangu na adui wenu kuwa marafiki wandani mkiwapa mapenzi, na hali wamekwishakufuru yaliyokujieni ya haki; [Al-Mumtahinah: 1]
Mpaka mwisho wa Suwrah.
Na Aayah nyenginezo zisizokuwa hizo, kisha Anasema tena Allaah (سبحانه وتعالى) katika kuweka masharti ya kumfuata Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾ قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٣٢﴾
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. Sema: Mtiini Allaah na Rasuli, lakini mkikengeuka basi hakika Allaah Hapendi makafiri. [Aal-‘Imraan: 31 – 32]
Na katika Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((ثَلاَثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ حَلاَوَةَ الإِيمَانِ: أَنْ يَكُونَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سِوَاهُمَا، وَأَنْ يُحِبَّ الْمَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إِلاَّ لِلَّهِ, وَأَنْ يَكْرَهَ أَنْ يَعُودَ فِي الْكُفْرِ كَمَا يَكْرَهُ أَنْ يُقْذَفَ فِي النَّارِ)) متفق عليه
Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata utamu wa imaan: Allaah na Rasuli Wake wawe vipenzi zaidi kwake kuliko wengineo, ampende mtu na wala asimpende isipokuwa kwa ajili ya Allaah, na achukie kurudi katika ukafiri baada ya Allaah kumwokoa kutoka huko kama anavyochukia kuingizwa motoni. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na pia,
عَنْ أَنَسٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَلَدِهِ وَوَالِدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ)) أَخْرَجَاهُ
Imepokewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mmoja wenu hawi Muumini mpaka anipende mimi kuliko watoto wake na baba yake na watu wote)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na haya aliyokuja nayo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni khabari kutoka kwa Allaah na ni amri Yake kwa vile Anavyovipenda Allaah na kuviridhia, pia ni katazo juu ya vile Aanavyovichukia na kuvikataa, basi mja akifuata yale Aliyoyaamrisha Allaah, na kujiepusha na yote Aliyoyakataza Allaah, hata kama yanaenda kinyume na matamanio yake, basi mtu huyo atakuwa Muumini wa kweli, ikiwa hatamani ispokuwa mwongozo huo. Na katika Hadiyth:
عَنِ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ، عن النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قال: إِنَّ أَوْثَقَ عُرَى الْإِيمَانِ: أَنْ تُحِبَّ فِي اللهِ، وَتُبْغِضَ فِي اللهِ. أحمد وحسنه الألباني في "صحيح الترغيب (3030) .
Amesimulia Al-Baraa Bin ‘Aazib kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kifungo Madhubuti cha Iymaan ni kumpenda Allaah na kuchukua Anayoyachukia.” [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (3030)]
Na pia,
عَن ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: "مَنْ أَحَبَّ فِي اللَّهِ، وَأَبْغَضَ فِي اللَّهِ، وَوَالَى فِي اللَّهِ، وَعَادَى فِي اللَّهِ، فَإِنَّمَا تُنَالُ وَلَايَةُ اللَّهِ بِذَلِكَ، وَلَنْ يَجِدَ عَبْدٌ طَعْمَ الْإِيمَانِ وَإِنْ كَثُرَتْ صَلَاتُهُ وَصَوْمُهُ حَتَّى يَكُونَ كَذَلِكَ. وَقَدْ صَارَتْ عَامَّةُ مُؤَاخَاةِ النَّاسِ عَلَى أَمْرِ الدُّنْيَا، وَذَلِكَ لَا يُجْدِي عَلَى أَهْلِهِ شَيْئاً" رَوَاهُ بنُ جَرِيرٍ
Ibn ‘Abaas (رضي الله عنهما) amesema: Atakayependa kwa ajili ya Allaah na Akachukia kwa ajili ya Allaah, na Akafanya urafiki kwa ajili ya Allaah na akafanya uadui kwa ajili ya Allaah, basi atapata mapenzi na ulinzi wa Allaah. Na mja hatopata kuonja Iymaan hata ikiwa Swalaah zake na Swawm zake zimekithiri, mpaka iwe hivyo. Imekuwa ni kawaida ya watu kufanya undugu kwa ajili ya maslahi ya mambo ya dunia na hayo hayatamfaa kitu mtu kwa watu wake. [Ibn Jariyr]
Amesema Hassan Al-Baswariy na wengineo katika Salaf: ‘’Walidai watu fulani kumpenda Allaah Allaah (عز وجل) Akawatahini kwa Aayah hii:
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Aal-‘Imraan: 31]
Na katika Hadiyth:
عَنْ أَبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((كُلُّ أُمَّتِي يَدخُلُونَ الجَنَّةَ إلا مَنْ أبَى)). قيلَ: وَمَنْ يَأبَى يَا رَسُول الله؟ قَالَ: ((مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أبَى)). رواه البخاري
Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ummah wangu wote wataingia Jannah isipokuwa atakayekataa.” Akaulizwa: Ni yupi atakayekataa Ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: “Atakayenitii mimi ataingia Jannah, na atakayeniasi basi amekataa.” [Al-Bukhaariy]
Na pia,
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبَادَةَ، أَخْبَرَنَا يَزِيدُ، حَدَّثَنَا سَلِيمُ بْنُ حَيَّانَ ـ وَأَثْنَى عَلَيْهِ ـ حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ مِينَاءَ، حَدَّثَنَا أَوْ، سَمِعْتُ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، يَقُولُ جَاءَتْ مَلاَئِكَةٌ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ نَائِمٌ فَقَالَ بَعْضُهُمْ إِنَّهُ نَائِمٌ. وَقَالَ بَعْضُهُمْ إِنَّ الْعَيْنَ نَائِمَةٌ وَالْقَلْبَ يَقْظَانُ. فَقَالُوا إِنَّ لِصَاحِبِكُمْ هَذَا مَثَلاً فَاضْرِبُوا لَهُ مَثَلاً. فَقَالَ بَعْضُهُمْ إِنَّهُ نَائِمٌ. وَقَالَ بَعْضُهُمْ إِنَّ الْعَيْنَ نَائِمَةٌ وَالْقَلْبَ يَقْظَانُ. فَقَالُوا مَثَلُهُ كَمَثَلِ رَجُلٍ بَنَى دَارًا، وَجَعَلَ فِيهَا مَأْدُبَةً وَبَعَثَ دَاعِيًا، فَمَنْ أَجَابَ الدَّاعِيَ دَخَلَ الدَّارَ وَأَكَلَ مِنَ الْمَأْدُبَةِ، وَمَنْ لَمْ يُجِبِ الدَّاعِيَ لَمْ يَدْخُلِ الدَّارَ وَلَمْ يَأْكُلْ مِنَ الْمَأْدُبَةِ. فَقَالُوا أَوِّلُوهَا لَهُ يَفْقَهْهَا فَقَالَ بَعْضُهُمْ إِنَّهُ نَائِمٌ. وَقَالَ بَعْضُهُمْ إِنَّ الْعَيْنَ نَائِمَةٌ وَالْقَلْبَ يَقْظَانُ. فَقَالُوا فَالدَّارُ الْجَنَّةُ، وَالدَّاعِي مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم فَمَنْ أَطَاعَ مُحَمَّدًا صلى الله عليه وسلم فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ، وَمَنْ عَصَى مُحَمَّدًا صلى الله عليه وسلم فَقَدْ عَصَى اللَّهَ، وَمُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم فَرْقٌ بَيْنَ النَّاسِ.
Amesimulia Sa‘iyd bin Miynaa’ kuwa amemsikia Jaabir bin ‘Abdillahi (رضي الله عنهما) akisema: Baadhi ya Malaika walikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa amelala. Baadhi yao wakasema: Hakika yeye amelala. Na wengine wakasema: Hakika macho yake yamelala na moyo wake uko macho. Wakasema: Kuna mfano kwa sahibu wenu huyu. Mmoja wao akasema: Kwa hiyo, upige mfano kwake. Wakasema baadhi yao: Hakika yeye amelala. Na wengine wakasema: Hakika macho yake yamelala lakini moyo wake uko macho. Wakasema: Mfano wake ni kama mfano wa mtu aliyejenga nyumba, kisha akafanya karamu, naye akatuma mwalikaji (mjumbe) kuwaalika watu. Kwa hivyo, yeyote aliyeukubali mwaliko wa mwalikaji, aliingia nyumbani na akala katika karamu iliyoandaliwa; na yeyote ambaye hakukubali mwaliko wa mwalikaji, hakuingia nyumbani, wala hakula katika karamu. Kisha Malaika wakasema: Ufasiri huu mfano kwake ili aufahamu. Baadhi yao wakasema: Hakika yeye amelala. Wengine wakasema: Hakika macho yake yamelala lakini moyo wake uko macho. Kisha wakasema: Nyumba ni Jannah, muitaji (mwalikaji) ni (Nabiy) Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Yeyote atayemtii Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hakika amemtii Allaah; na yeyote atayemuasi Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hakika amemuasi Allaah. Na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amewatenganisha watu (yaani kwa ujumbe wake, mwema ametofautiana na mbaya na vile vile Muumini ni tofauti na kafiri) [Al-Bukhaariy]
Kutokea hapa inatambulika kwamba haitimii ‘’Shahaadah ya
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ
ila ipatikane na Shahaadah ya
مُحَمدا رَسُول الله
Muhamaadan Rasuwlu Allaah
Na ikishajulikana kwamba hayatimii mapenzi ya Allaah (عز وجل) mpaka kipendwe kile Anachokipenda Yeye na mpaka kichukiwe Anachokichukia Yeye, hapo itakuwa hakuna njia ya kujua Anavyovipenda Allaah na kuviridhia, na hakuna njia ya kutambua Anavyovichukia Allaah, ila kwa kufuata yale anayoamrisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kujiepusha na vile anavyovikataza. Kwahiyo ikawa mapenzi ya Allaah yanalazimiana na mapenzi ya kumpenda Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kumsadikisha na kumfuata, kwa sababu hii, ndio Allaah Amekutanisha mapenzi yake na mapenzi ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika sehemu nyingi ndani ya Qur-aan, kama vile kauli yake Allaah (عزَّ وجلّ)
قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٢٤﴾
Sema: Ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake (au waume) zenu na jamaa zenu na mali mliyoichuma na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake, na majumba mnayoridhika nayo, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Rasuli Wake na kufanya jihaad katika njia Yake; basi ngojeeni mpaka Allaah Alete Amri Yake (ya adhabu). Na Allaah Haongoi watu mafasiki. [At-Tawbah: 24]