033-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Ahzaab Aayah 35: إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 35
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾
35. Hakika Waislamu wanaume na wanawake, na Waumini wanaume na wanawake, na watiifu wanaume na wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao swadaqah wanaume na wanawake, na wafungao Swawm wanaume na wanawake, wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanaomdhukuru Allaah kwa wingi wanaume na wanawake; Allaah Amewaandalia maghfirah na ujira adhimu”. [Al-Ahzaab (33): 35]
Sababun-Nuzuwl:
حَدَّثَنَا عَبْدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ حُسَيْنٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ أُمِّ عُمَارَةَ الأَنْصَارِيَّةِ، أَنَّهَا أَتَتِ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ مَا أَرَى كُلَّ شَيْءٍ إِلاَّ لِلرِّجَالِ وَمَا أَرَى النِّسَاءَ يُذْكَرْنَ بِشَيْءٍ فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ : إن الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ الآيَةَ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ وَإِنَّمَا يُعْرَفُ هَذَا الْحَدِيثُ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ
Ametuhadithia ‘Abdu bin Humayd, ametuhadithia Muhammad bin Kathiyr, ametuhadithia Sulaymaan bin Kathiyr, toka kwa Huswayn, toka kwa ‘Ikrimah, toka kwa Ummu ‘Ammaarah Al-Answaariyyah kuwa alimwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumwambia: Sioni kila kitu isipokuwa ni kwa wanaume tu, na sioni wanawake wakitajwa kwa lolote. Hapo ikateremka Aayah hii:
إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾
Hakika Waislamu wanaume na wanawake, na Waumini wanaume na wanawake, na watiifu wanaume na wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao swadaqah wanaume na wanawake, na wafungao Swawm wanaume na wanawake, wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanaomdhukuru Allaah kwa wingi wanaume na wanawake; Allaah Amewaandalia maghfirah na ujira adhimu”. [Al-Ahzaab (33): 35]
Abuu ‘Iysaa amesema: Hadiyth hii ni Hasan Ghariyb, nayo kwa hakika inajulikana kwa picha hii.
[At-Tirmidhiy katika Mujallad wa 4 ukurasa wa 116]
Al-Haakim katika Mujallad wa 2 ukurasa wa 416 amekhariji mfano wake toka Hadiyth ya Ummu Salamah, na kusema ni Swahiyh juu ya sharti ya Masheikh Wawili ambao hawakuikhariji, na Adh-Dhahabiy ameikubali. Lakini Mujaahid ni mwingi wa kusimulia Riwaayah toka kwa Swahaba ambao yeye hakuzisikia toka kwao. Hivyo haijulikani kama ameisikia toka kwa Ummu Salamah au laa. At-Twabaraaniy naye amekhariji mfano wake toka Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas. Al-Haythamiy amesema katika Majma’u Az-Zawaaid Mujallad wa 7 ukurasa wa 91: “Yupo Qaabuws, na yeye ni mdhaifu wa kumbukumbu, lakini ameaminiwa. Kisha nimemwona Al-Haafidh Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) akiwa ametaja Isnaad nyingine mbili kwa Hadiyth ya Ummu Salamah katika Mujallad wa 3 ukurasa wa 47 wa Tafsiyr yake. Allaah Amlipe jazaa njema kwa pupa yake ya kukusanya Asaaniyd za Hadiyth.”