01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Haya na Fadhila Zake na Kuhimizwa Kuwa na Maadili Hayo
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الحياء وفضله والحث على التخلق به
01-Mlango Wa Haya na Fadhila Zake na Kuhimizwa Kuwa na Maadili Hayo
Hadiyth – 1
عن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرَّ عَلَى رَجُلٍ مِنَ الأنْصَار وَهُوَ يَعِظُ أخَاهُ في الحَيَاءِ ، فَقَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( دَعْهُ ، فَإنَّ الْحَيَاءَ مِنَ الإيمَانِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipota kwa mtu fulani miongoni mwa Answaar, naye alikuwa anamuonya ndugu yake katika haya. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Mwache kwani kuwa na haya ni katika Iymaan." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, Abu Daawuud, An-Nasai na Malik].
Hadiyth – 2
وعن عمران بن حصينٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( الْحَيَاءُ لاَ يَأْتِي إِلاَّ بِخَيْرٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية لمسلمٍ : (( الحياءُ خَيْرٌ كُلُّهُ )) أَوْ قَالَ : (( الْحَيَاءُ كُلُّهُ خَيْرٌ )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haya haileti isipokuwa kheri." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud].
Katika Riwaayah ya Muslim: "Haya ni kheri yote" au amesema: "Haya yote ni kheri."
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الإيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ أَوْ بِضْعٌ وَسِتُّونَ شُعْبَةً : فَأفْضَلُهَا قَوْلُ : لاَ إلهَ إِلاَّ الله ، وَأدْنَاهَا إمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ ، وَالحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنَ الإيمَانِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Iymaan ina sehemu sitini. Iliyo bora zaidi ni kauli ya Laa Ilaaha Illa Allaah (Hapana anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah) na ya chini kabisa ni kuondosha chenye kuudhi njiani. Na kuwa na haya ni sehemu ya Iymaan." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hadiyth – 4
وعن أَبي سعيدٍ الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم أشَدَّ حَيَاءً مِنَ العَذْرَاءِ في خِدْرِهَا ، فَإذَا رَأَى شَيْئاً يَكْرَهُهُ عَرَفْنَاهُ في وَجْهِه . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudhry (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikua ni mtu mwenye haya sana kuliko mwanamwari chumbani kwake, akiona kitu anachokichukia tunajua kupitia usoni mwake." [Al-Bukhaariy na Muslim]