02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuhifadhi Siri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

بابُ حفظ السِّر

02-Mlango Wa Kuhifadhi Siri

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا ﴿٣٤﴾

Na timizeni ahadi; hakika ahadi itakuwa ni ya kuulizwa. [Al-Israa: 34]

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ مِنْ أشَرِّ النَّاسِ عِنْدَ اللهِ مَنْزِلَةً يَوْمَ القِيَامَةِ الرَّجُلَ يُفْضِي إِلَى الْمَرْأةِ وتُفْضِي إِلَيْهِ ، ثُمَّ يَنْشُرُ سِرَّهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika watu waovu kabisa kwa daraja mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah ni mtu aliyejamiiana na mkewe na mke aliyestarehe na mumewe kisha mmoja wao akatangaza siri hiyo." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن عبدِ الله بن عمر رضي الله عنهما : أنَّ عمرَ رضي الله عنه حِيْنَ تأيَّمَتْ بِنْتُهُ حَفْصَةُ ، قَالَ : لَقِيتُ عُثْمَانَ بْنَ عَفّانَ رضي الله عنه ، فَعَرَضْتُ عَلَيْهِ حَفْصَةَ ، فَقُلْتُ : إنْ شِئْتَ أَنْكَحْتُكَ حَفْصَةَ بِنْتَ عُمَرَ ؟ قَالَ : سأنْظُرُ فِي أمْرِي . فَلَبِثْتُ لَيَالِيَ ثُمَّ لَقِيَنِي ، فَقَالَ : قَدْ بَدَا لِي أنْ لاَ أتَزَوَّجَ يَوْمِي هَذَا . فَلَقِيتُ أَبَا بَكْرٍ رضي الله عنه ، فقلتُ : إنْ شِئْتَ أنْكَحْتُكَ حَفْصَةَ بنْتَ عُمَرَ ، فَصَمتَ أَبُو بَكْرٍ رضي الله عنه ، فَلَمْ يَرْجِعْ إلَيَّ شَيْئاً ! فَكُنْتُ عَلَيْهِ أوْجَدَ مِنِّي عَلَى عُثْمَانَ ، فَلَبِثَ لَيَالِيَ ثُمَّ خَطَبَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، فَأنْكَحْتُهَا إيَّاهُ . فَلَقِيَنِي أَبُو بَكْرٍ ، فَقَالَ : لَعَلَّكَ وَجَدْتَ عَلَيَّ حِيْنَ عَرَضْتَ عَلَيَّ حَفْصَةَ فَلَمْ أرْجِعْ إِلَيْكَ شَيْئاً ؟ فقلتُ : نَعَمْ ، قَالَ : فَإنَّهُ لَمْ يَمْنَعْنِي أنْ أرْجِعَ إِلَيْك فِيمَا عَرَضْتَ عَلَيَّ إِلاَّ أنِّي كُنْتُ عَلِمْتُ أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ذَكَرَهَا ، فَلَمْ أكُنْ لأُفْشِيَ سِرَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، وَلَوْ تَرَكَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم لَقَبِلْتُهَا . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ya kwamba pindi Hafswah bint 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhaa) alipoachwa mjane (kufa mumewe), 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikutana na 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) na kumwambia: "Ukitaka nitakuoza bint yangu, Hafswah." Akasema: "Nitaangalia jambo hilo." Akakaa kwa siku kadhaa, kisha akakutana na 'Umar na kumwambia: "Nimefikiria juu ya mas-ala hayo na naona kuwa sitaowa hivi karibuni." Baada ya hapo nilikutana na Abu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) nikasema: "Ukitaka nitakuoza Hafswah bint 'Umar." Abu Bakr alikaa kimya na wala hakunijibu chochote. Jambo hili liliniuma zaidi kuliko jawabu la 'Uthmaan. Nilikaa kwa siku chache mara Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaleta posa na mimi nukamuozesha. Akakutana nami Abu Bakr, ambaye aliniambia: "Huenda ukawa hukufurahi wakati ulipotaka nimuoe Hafswah, nami sikukujibu lolote." Nikasema: "Ndio." Akasema: "Hakika hakuna kilicho nizuia mimi kukubali hilo ila nilijua ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa tayari amemtaja (kwa nia ya kumuoa). Na sikuweza kutoa siri ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na lau Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asingemuoa basi mimi ningekubali maombi yako hayo." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كُنَّ أزْوَاجُ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم عِنْدَهُ ، فَأقْبَلَتْ فَاطِمَةُ رضي الله عنها تَمْشِي ، مَا تُخْطِئُ مِشيتُها مِنْ مشْيَةِ رسول الله صلى الله عليه وسلم شَيْئاً ، فَلَمَّا رَآهَا رَحَّبَ بِهَا ، وقال : (( مَرْحَباً بابْنَتِي )) ، ثُمَّ أجْلَسَهَا عَنْ يَمِينِهِ أَوْ عَنْ شِمَالِهِ ، ثُمَّ سَارَّهَا فَبَكتْ بُكَاءً شَديداً ، فَلَمَّا رَأى جَزَعَهَا ، سَارَّهَا الثَّانِيَةَ فَضَحِكَتْ ، فقلتُ لَهَا : خَصَّكِ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم مِنْ بَيْنِ نِسَائِهِ بالسِّرَارِ ، ثُمَّ أنْتِ تَبْكِينَ ! فَلَمَّا قَامَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم سَألْتُهَا : مَا قَالَ لَكِ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ؟ قالت : مَا كُنْتُ لأُفْشِي عَلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم سِرَّهُ ، فَلَمَّا تُوُفِّيَ رسول الله صلى الله عليه وسلم قُلْتُ : عَزَمْتُ عَلَيْكِ بِمَا لِي عَلَيْكِ مِنَ الحَقِّ ، لَمَا حَدَّثْتِنِي مَا قَالَ لَكِ رسول الله صلى الله عليه وسلم ؟ فقالتْ : أمَّا الآن فَنَعَمْ ، أمَّا حِيْنَ سَارَّنِي في المَرَّةِ الأُولَى فأخْبَرَنِي أنّ جِبْريلَ كَانَ يُعَارِضُهُ القُرآنَ في كُلِّ سَنَةٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ، وَأنَّهُ عَارَضَهُ الآنَ مَرَّتَيْنِ ، وَإنِّي لا أُرَى الأجَلَ إِلاَّ قَدِ اقْتَرَبَ ، فَاتَّقِي اللهَ وَاصْبِرِي ، فَإنَّهُ نِعْمَ السَّلَفُ أنَا لَكِ ، فَبَكَيْتُ بُكَائِي الَّذِي رَأيْتِ ، فَلَمَّا رَأى جَزَعِي سَارَّنِي الثَّانِيَةَ ، فَقَالَ : (( يَا فَاطِمَةُ ، أمَا تَرْضَيْنَ أنْ تَكُونِي سَيِّدَةَ نِسَاءِ المُؤُمِنِينَ ، أَوْ سَيَّدَةَ نِساءِ هذِهِ الأُمَّةِ ؟ )) فَضَحِكتُ ضَحِكِي الَّذِي رَأيْتِ . متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Sote wake wa Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tuko naye wakati mmoja mara akaja Faatwimah. Utembeaji wake ulikuwa kama ule wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Alipomuona alimkaribisha kwa kumwambia: "Karibu, bint yangu." Kisha akamkalisha uapande wake wa kulia au wa kushoto kisha kumnong'oneza kitu ambacho kilimliza sana. Alipomwuona na huzuni kubwa, alimnog'oneza mara ya pili, naye akacheka. Nikamuliza: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewapuuza wakeze wote na kuzungumza nawe kwa siri, kisha wewe ukalia." Alipoondoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nilimuuliza: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekuambia nini?" Akasema: "Siwezi kutoa siri ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Alipoaga dunia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nilimuuliza: "Nakuomba kwa jina la Allaah kwa ile haki niliyo nayo juu yako, uniambie ni jambo gani alilokuambia Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Ama sasa naweza kukuambia. Hakika pale aliponionong'oneza mara ya kwanza alinipasha habari kuwa: 'Jibriyl alikuwa kila mwaka akimsomea na kisha akimsikiliza Qur-aan mara moja au mara mbili. Na ama sasa anafanya hivyo mara mbili. Na hakika naona kuwa wakati wangu umefika. Hivyo, mche Allaah na usubiri, kwani hakika mimi ni mtangulizi mwema kwako. Nililia kilio changu ulivyoona. Alipoona huzuni yangu, aliniong'oneza mara ya pili akasema: "Ee Faatwimah! Huridhiki kuwa wewe bibi wa ummah huu?' Nikacheka kicheko changu ulivyoona." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن ثَابِتٍ ، عن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : أتَى عَلَيَّ رسول الله r وَأنَا ألْعَبُ مَعَ الغِلْمَانِ ، فَسَلمَ عَلَيْنَا ، فَبَعَثَني إِلَى حاجَةٍ ، فَأبْطَأتُ عَلَى أُمِّي . فَلَمَّا جِئْتُ ، قالت : مَا حَبَسَكَ ؟ فقلتُ : بَعَثَني رسولُ الله صلى الله عليه وسلم لِحَاجَةٍ ، قالت : مَا حَاجَتُهُ ؟ قُلْتُ : إنَّهاَ سرٌّ . قالت : لا تُخْبِرَنَّ بِسرِّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أحَداً ، قَالَ أنَسٌ : وَاللهِ لَوْ حَدَّثْتُ بِهِ أحَداً لَحَدَّثْتُكَ بِهِ يَا ثَابِتُ . رواه مسلم وروى البخاري بعضه مختصراً .

Imepokewa kutoka kwa Thaabit kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alinijia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nilikuwa ninachezsa na watoto, Alitusalimia akanituma haja, hivyo nikachelewa kwa mamangu. Nilipofika nyumbani , akaniuliza: "Nini kimekuchelewesha?" Nikasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinituma haja." Akasema: "Ni haja gani?" Nikasema: "Hiyo ni siri." Akaniambia: "Usimwambie yoyote siri ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ." Akasema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Naapa kwa Allaah! Lau ningekuwa ni mwenye kufichua siri hiyo kwa yeyote basi ningekueleza wewe, ee Thaabit." [Muslim, na Al-Bukhaariy amenukuu baadhi yake kwa mukhtasar]

 

 

 

Share