03-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kutekeleza Ahadi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الوفاء بالعهد وَإنجاز الوَعد

03-Mlango Wa Kutekeleza Ahadi

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا ﴿٣٤﴾

Na timizeni ahadi; hakika ahadi itakuwa ni ya kuulizwa. [Al-Israa: 34]

 

وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ ﴿٩١﴾

Na timizeni ahadi ya Allaah mnapoahidi. [An-Nahl: 91]

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ ۚ  ﴿١﴾

Enyi walioamini! Timizeni mikataba. [Al-Maaidah: 1]

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾

Enyi walioamini!  Kwanini mnasema yale msiyoyafanya? Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya. [Asw-Swaff: 2-3]

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( آيَةُ المُنَافِقِ ثَلاَثٌ : إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ ، وَإِذَا وَعَدَ أخْلَفَ ، وَإِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Alama za mnafiki ni tatu: Anapozungumza anasema uwongo; na anapoahidi huvunja ahadi; na anapoaminiwa hufanya hiyana." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنَافِقاً خَالِصاً ، وَمَنْ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْهُنَّ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنَ النِّفَاقِ حَتَّى يَدَعَهَا : إِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ ، وَإِذَا حَدَّثَ كَذَبَ ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ ، وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdilaah bin 'Amruu bin Al-'Aas (Radhwiya Allahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu yeyote akiwa na mambo manne atakuwa mnafiki hasa, na kama atakuwa na moja katika hayo manne: atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aliache. Akiaminiwa hufanya hiyana; na akizungumza anaongopa; na anapotoa ahadi huvunja na anapogombana anaiacha haki kuwa jeuri." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( لَوْ قَدْ جَاءَ مَالُ الْبَحْرَيْنِ أعْطَيْتُكَ هكَذَا وَهَكَذَا وَهكَذَا )) فَلَمْ يَجِئْ مَالُ الْبَحْرَينِ حَتَّى قُبِضَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، فَلَمَّا جَاءَ مَالُ الْبَحْرَيْنِ أمَرَ أَبُو بَكْرٍ رضي الله عنه فَنَادَى : مَنْ كَانَ لَهُ عِنْدَ رسول الله صلى الله عليه وسلم عِدَةٌ أَوْ دَيْنٌ فَلْيَأتِنَا ، فَأتَيْتُهُ وَقُلْتُ لَهُ : إنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ لي كَذَا وَكَذَا ، فَحَثَى لي حَثْيَةً فَعَدَدْتُهَا ، فَإذَا هِيَ خَمْسُمِئَةٍ ، فَقَالَ لِي : خُذْ مِثْلَيْهَا . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema aliniambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Lau mali ya Bahrayn itakuja basi nitakupatia hivi na hivi." Mali ya Bahrayn haikuja mpaka akafariki Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ilipokuja mali kutoka Bahrayn Abu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliamuru kutangazwe: 'Ambaye ana ahadi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), au anayemdai aje kwetu. Nilifika kwake na kumwambia: "Hakika Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia hivi na vile." Abu Bakr alinichotea fedha Nilipozihesabu zilikuwa ni Dirhamu mia tano. Kisha akaniambia: "Chukua mfano wake mara mbili." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share