06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kubainisha Maneno na Kuweza Wazi kwa Mwenye Kusikiliza na Kuyakariri Ili Apate Kufahamu Ikiwa Hatafahamu Ila Kwayo
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب بيان الكلام وإيضاحه للمخاطب وتكريره ليفهم إذا لَمْ يفهم إِلا بذلك
06-Mlango Wa Kupendeza Kubainisha Maneno na Kuweza Wazi kwa Mwenye Kusikiliza na Kuyakariri Ili Apate Kufahamu Ikiwa Hatafahamu Ila Kwayo
Hadiyth – 1
عن أنسٍ رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا تَكَلَّمَ بِكَلِمَةً أعَادَهَا ثَلاَثاً حَتَّى تُفْهَمَ عَنْهُ ، وَإِذَا أتَى عَلَى قَوْمٍ فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ سَلَّمَ عَلَيْهِمْ ثَلاثاً . رواه البخاري .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akizungumza alikuwa akirudia maneno mara tatu mpaka afahamike. Na alipokuwa akija kwa watu na kuwasalimia husalimia mara tatu." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ كَلاَمُ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَلاماً فَصْلاً يَفْهَمُهُ كُلُّ مَنْ يَسْمَعُهُ . رواه أَبُو داود .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)Alikuwa akizungumza kwa uwazi kabisa hivyo akifahamika na kila mmoja mwenye kumsikia." [Abu Daawuud]