07-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Mtu Kumsikiliza aliyekaa Nae Ambayo Sio Haramu, na Kumsikiliza Mwanazuoni na Mtoa Waadhi Mbele ya Mkutano Wake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب إصغاء الجليس لحديث جليسه الذي ليس بحرام واستنصات العالم والواعظ حاضري مجلسه
07-Mlango Wa Mtu Kumsikiliza aliyekaa Nae Ambayo Sio Haramu, na Kumsikiliza Mwanazuoni na Mtoa Waadhi Mbele ya Mkutano Wake
عن جرير بن عبدِ اللهِ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم في حَجَّةِ الْوَدَاعِ : (( اسْتَنْصِتِ النَّاسَ )) ثُمَّ قَالَ : (( لاَ تَرْجِعُوا بَعْدِي كُفّاراً يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Jariyr bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Aliniambia mimi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hajjatul Wadaa'i (Hijjah ya kuaga): "Wanyamazishe watu." Kisha akasema: "Msirudi baada yangu katika ukafiri kwa kuuana nyinyi kwa nyinyi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
