08-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kutorefusha Mawaidha
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
بابُ الوَعظ والاقتصاد فِيهِ
08-Mlango Wa Kutorefusha Mawaidha
قَالَ الله تَعَالَى:
ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ ﴿١٢٥﴾
Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. [An-Nahl: 125]
Hadiyth – 1
وعن أَبي وائلٍ شقيقِ بن سَلَمَةَ ، قَالَ : كَانَ ابنُ مَسْعُودٍ رضي الله عنه يُذَكِّرُنَا في كُلِّ خَمِيسٍ ، فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ : يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمانِ ، لَوَدِدْتُ أنَّكَ ذَكَّرْتَنَا كُلَّ يَوْمٍ ، فَقَالَ : أمَا إنَّهُ يَمْنَعُنِي مِنْ ذَلِكَ أنَّي أكْرَهُ أنْ أُمِلَّكُمْ ، وَإنِّي أتَخَوَّلُكُمْ بِالْمَوْعِظَةِ ، كَمَا كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَتَخَوَّلُنَا بِهَا مَخَافَةَ السَّآمَةِ عَلَيْنَا . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Wa'il Shaqiyq bin Salamah amesema: Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) Alikuwa akitupatia mawaidha kila siku ya Alkhamisi. Mtu mmoja akamwambia yeye: "Ee Abu 'Abdur-Rahman! Natamani uwe unatupatia mawaidha kila siku." Akasema: "Hakika linalo nikataza mimi kufanya hivyo ni kuogopea kuwachosha kwa mawaidha. Mimi ninafanya kama alivyokuwa akifanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kutuogopea tusije tukachoka." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
Hadiyth – 2
وعن أَبي اليقظان عمار بن ياسر رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّ طُولَ صَلاَةِ الرَّجُلِ ، وَقِصَرَ خُطْبَتِهِ ، مَئِنَّةٌ مِنْ فِقههِ ، فأطِيلُوا الصَّلاَةَ وَأقْصِرُوا الْخُطْبَةَ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abul Yaqdhaan 'Ammaar bin Yaasir (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika mtu kurefusha Swalaah na kufupisha khutbah inayonyesha umahiri na alama ya ujuzi wake. Hivyo refusheni Swalaah na fupisheni khutbah." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن مُعاوِيَة بن الحكم السُّلَمي رضي الله عنه ، قَالَ : بَيْنَا أنَا أُصَلّي مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، إذْ عَطَسَ رَجُلٌ مِنَ القَوْمِ ، فَقُلْتُ : يَرْحَمُكَ اللهُ ، فَرَمَانِي القَوْمُ بِأبْصَارِهِمْ ! فَقُلْتُ : وَاثُكْلَ أُمِّيَاهُ ، مَا شَأنُكُمْ تَنْظُرُونَ إلَيَّ ؟! فَجَعَلُوا يَضْرِبُونَ بأيديهم عَلَى أفْخَاذِهِمْ ! فَلَمَّا رَأيْتُهُمْ يُصَمِّتُونَنِي لكِنّي سَكَتُّ ، فَلَمَّا صَلّى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَبِأبِي هُوَ وَأُمِّي ، مَا رَأيْتُ مُعَلِّماً قَبْلَهُ وَلاَ بَعْدَهُ أحْسَنَ تَعْلِيماً مِنْهُ ، فَوَاللهِ مَا كَهَرَني ، وَلاَ ضَرَبَنِي ، وَلاَ شَتَمَنِي . قَالَ : (( إنَّ هذِهِ الصَّلاَةَ لاَ يَصْلُحُ فِيهَا شَيْءٌ مِنْ كَلامِ النَّاسِ ، إنَّمَا هِيَ التَّسْبِيحُ وَالتَّكْبِيرُ ، وَقِراءةُ القُرْآنِ )) ، أَوْ كَمَا قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم . قلتُ : يَا رسول الله ، إنّي حَدِيثُ عَهْدٍ بِجَاهِلِيَّةٍ ، وَقَدْ جَاءَ اللهُ بِالإسْلاَمِ ، وَإنَّ مِنّا رِجَالاً يَأتُونَ الْكُهّانَ ؟ قَالَ : (( فَلاَ تَأتِهِمْ )) قُلْتُ : وَمِنّا رِجَالٌ يَتَطَيَّرُونَ ؟ قَالَ : (( ذَاكَ شَيْء يَجِدُونَهُ في صُدُورِهِمْ فَلاَ يَصُدَّنَّهُمْ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Mu'awiyah bin Al-Hakam As-sulamiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nikiwa naswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mtu katika jamaa akacheua nikasema: "yarhamuka Allaah (Allaah Akurehemu)." Watu wakanikodolea macho. Nikasema: "Mama zenu wapotee! Mna nini mnaniangalia hivi?", wakawa wanapiga kwa mikono mapaja yao. Nilipowaona wakininyamazisha, basi nilinyamaza. Alipomaliza Swalaah Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), baba yangu na mama yangu wawe fidia kwake, sijaona mwalimu mzuri kuliko yeye kabla wala baada yake. Naapa kwa Allaah! Hakunilaumu wala hakunipiga wala hakunitukana. Alisema: "Hakika hii Swalaah, haifai ndani yake maneno ya watu. Kwa hakika hiyo ni tasbihi , takbiri na kusoma Qur-aan", au kama alivyosema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi ni hivi karibuni tu nimetoka katika Ujahiliyah, na Allaah ametuletea Uislaamu. Na katika sisi kuna watu wanaendea makuhani." Akasema: "Msiende kwao." Nikasema: "Miongoni mwetu wako wanao ongozwa na bahati." Akasema: "Hilo ni jambo wanaolipata katika vifua vyao (na akili zao). Wasiwazuie." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن العِرْباض بن ساريَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : وَعَظَنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنْهَا القُلُوبُ ، وَذَرَفَتْ مِنْهَا العُيُونُ ... وَذَكَرَ الحَدِيثَ وَقَدْ سَبَقَ بِكَمَالِهِ في باب الأمْر بِالمُحَافَظَةِ عَلَى السُّنَّة ، وَذَكَرْنَا أنَّ التَّرْمِذِيَّ ، قَالَ : (( إنّه حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Irbaadh bin Saariyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Alituaidhia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mawaidha yaliyozifanya nyoyo zikaingia hofu na macho yakabubujikwa na machozi. Na akitaja hiyo Hadiyth ambayo imetangulia kutafsiriwa katika mlango wa kuhifadhi Sunnah, [At-Tirmidhiy amesema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]