Imaam Hasan Al-Baswriy: Watu Wametahaniwa Kwa Kauli Ya Allaah Kumpenda Yeye Ni Kumfuata Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)
Watu Wametahaniwa Kwa Kauli Ya Allaah Kumpenda Yeye
Ni Kumfuata Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)
Imaam Hasan Al-Baswriy (Rahimahu Allaah)
Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-'Imraan: 31]
Hakika mapenzi ya Allaah ni kwa kumfuata Rasuli Wake. Kufuata (Itbaa’a) ni dalili ya mapenzi ya kwanza kabisa na ushuhuda wa mfano kabisa, hilo ni sharti la kuthibiti kwa mapenzi haya na bila ya hayo basi mapenzi ya ki- Shariy’ah hayawezi kufikiwa na haiwezekani kusawiri maanayake sahihi.
Amesema Imaam Hasan Al-Baswriy (Rahimahu Allaah) amesema na wengine katika Salaf: “Watu wamedai kuwa wanampenda Allaah, basi Allaah Akawapa mtihani kwa Aayah hii.”
[Tafsiyr Ibn Kathiyr 1/358]