07-Hadiyth Husnul-Khuluq: Husnul-Khuluq Ni Sababu Ya Kuingizwa Jannah
Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)
Hadiyth Ya 7
Husnul-Khuluq Ni Sababu Ya Kuingizwa Jannah
عن أَبِي هُرَيْرَةَ: سُئِلَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: مَا أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ الْجَنَّةَ؟ قَالَ: ((تَقْوَى اللهِ، وَحُسْنُ الْخُلُقِ)) قَالَ: وَمَا أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ النَّارَ؟ قَالَ: ((الأَجْوَفَانِ: الْفَمُ وَالْفَرْجُ.))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Jambo gani zaidi litakalokuwa ni sababu ya kumwingiza mtu Jannah?” Akasema: ((Taqwa (kumcha Allaah) na Husnul-Khuluq (tabia njema)). Na akulizwa: “Jambo gani zaidi litakalokuwa ni sababu ya kumwingiza mtu Motoni?” Akasema; ((Mdomo na sehemu za siri)) [Al-Adab Al-Mufrad, Swahiyh Ibn Maajah (3443)], Swahiyh At-At-Tirmidhiy (2004)]