08-Hadiyth Husnul-Khuluq: Amedhaminiwa Jannah (Pepo) Mwenye Husnul-Khuluq
Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)
Hadiyth Ya 8
Amedhaminiwa Jannah (Pepo) Mwenye Husnul-Khuluq
عَنْ أَبِي أُمَامَةَ البَاهِلي (رضي الله عنه) قَال: قَال رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَنَا زَعِيم بَيْت فِي رَبَض الْجَنَّة لِمَنْ تَرَكَ الْمِرَاء وَإِنْ كَانَ مُحِقًّا، وَبِبَيْتٍ فِي وَسَط الْجَنَّة لِمَنْ تَرَكَ الْكَذِب وَإِنْ كَانَ مَازِحًا، وَبِبَيْتٍ فِي أَعْلَى الْجَنَّة لِمَنْ حَسُنَ خُلُقه)) حديث صحيح رواه أبو داود بإسناد صحيح
Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mimi ni mdhamini wa nyumba ya kando ya Jannah kwa anayeacha mabishano [wenye shaka] hata kama ni mwenye haki, na ni mdhamini wa nyumba iliyo katikati ya Jannah kwa anayeacha uongo japo ni kwa mzaha, na mdhamini wa nyumba iliyo mahala pa juu zaidi ya Jannah kwa ambaye ana husnul-khuluq (tabia njema)). [Hadiyth Swahiyh ameipokea Abu Daawuwd isnaad yake ni Swahiyh]