11-Hadiyth Husnul-Khuluq: Wema Ni Katika Husnul-Khuluq
Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)
Hadiyth Ya 11
Wema Ni Katika Husnul-Khuluq
وعن النَّوَاس بنِ سمعان رضي الله عنه ، قَالَ : سألتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عن البِرِّ وَالإثم ، فَقَالَ : (( البِرُّ : حُسنُ الخُلقِ ، والإثمُ : مَا حاك في صدرِك ، وكَرِهْتَ أن يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa An-Nawwaas bin sam'aan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu wema na dhambi akasema: "Wema ni Husnul-Khuluq (Tabia njema) na dhambi ni iliokera nafsini mwako na ukachukia watu kuiona." [Muslim]