12-Hadiyth Husnul-Khuluq: Aliye Mbora Kabisa Ni Mwenye Husnul-Khuluq
Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)
Hadiyth Ya 12
Aliye Mbora Kabisa Ni Mwenye Husnul-Khuluq
عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : لَمْ يكن رسولُ الله صلى الله عليه وسلم فَاحِشاً وَلاَ مُتَفَحِّشاً ، وكان يَقُولُ : (( إنَّ مِنْ خِيَارِكُمْ أحْسَنَكُمْ أخْلاَقاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillah bin 'Amru bin Al-'aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Hakuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mwenye kuzungumza maneno machafu wala kuyasikiliza." Na alikuwa akisema: "Hakika aliye bora miongoni mwenu ni yule mwenye husnul-khuluq (tabia nzuri)" [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ahmad].