13-Hadiyth Husnul-Khuluq: Ujira Mara Mbili Kwa Kumfunza Husnul-Khuluq Kijakazi

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 13

 

Ujira Mara Mbili Kwa Kumfunza Husnul-Khuluq Kijakazi    

 

Alhidaaya.com

 

عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ إِذَا أَدَّبَ الرَّجُلُ أَمَتَهُ فَأَحْسَنَ تَأْدِيبَهَا، وَعَلَّمَهَا فَأَحْسَنَ تَعْلِيمَهَا ثُمَّ أَعْتَقَهَا فَتَزَوَّجَهَا، كَانَ لَهُ أَجْرَانِ، وَإِذَا آمَنَ بِعِيسَى ثُمَّ آمَنَ بِي، فَلَهُ أَجْرَانِ، وَالْعَبْدُ إِذَا اتَّقَى رَبَّهُ وَأَطَاعَ مَوَالِيَهُ، فَلَهُ أَجْرَانِ ‏"‏‏.‏

Imepokewa kwa Abu Muwsaa Al-Ash‘ariyy  (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Pindi mtu anapomfundisha adabu nzuri kabisa kijakazi wake, akamsomesha kwa kuboresha elimu yake, kisha akamuacha huru na kumuoa, atakuwa na ujira mara mbili. Na pindi mtu atakapomuamini ‘Iysaa, kisha akaniamimi mimi, naye atakuwa na ujira mara mbili. Na mtumwa atakapomcha Rabb wake (akawa na Taqwa) na akawatii mabwana zake, basi atakuwa na ujira mara mbili”. [Al-Bukhaariy]

 

Share