14-Hadiyth Husnul-Khuluq: Inawatosheleza Watu Husnul-Khuluq Kulikoni Mali
Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)
Hadiyth Ya 14
Inawatosheleza Watu Husnul-Khuluq Kulikoni Mali
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّكُمْ لَا تَسَعُونَ اَلنَّاسَ بِأَمْوَالِكُمْ، وَلَكِنْ لِيَسَعْهُمْ بَسْطُ اَلْوَجْهِ، وَحُسْنُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ أَبُو يَعْلَى، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Nyinyi hamuwezi kuwatosheleza watu kwa mali zenu, lakini iwatoshe wao kutoka kwenu uchangamfu wa uso na khulqa (tabia) njema.” [Imetolewa na Abuu Ya’laa na akaisahihisha Al-Haakim]