17-Hadiyth Husnul-Khuluq: Ee Allaah Niongoze Katika Husnul-Khuluq Na Niepushe Akhlaaq Mbaya
Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)
Hadiyth Ya 17
Ee Allaah Niongoze Katika Husnul-Khuluq Na Niepushe Akhlaaq Mbaya
Du’aa hii ni miongoni mwa du’aa za kufungulia Swalaah Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)
عَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ كَانَ إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ قَالَ "
‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa pindi anaposimama kuanza Swalaah alikuwa akiomba:
وَجَّهـتُ وَجْهِـيَ لِلَّذي فَطَرَ السَّمـواتِ وَالأَرْضَ حَنـيفَاً وَمـا أَنا مِنَ المشْرِكين، إِنَّ صَلاتـي، وَنُسُكي، وَمَحْـيايَ، وَمَماتـي للهِ رَبِّ العالَمين، لا شَريـكَ لَهُ وَبِذلكَ أُمِرْتُ وَأَنا مِنَ المسْلِـمين. اللّهُـمَّ أَنْتَ المَلِكُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْت، أَنْتَ رَبِّـي وَأَنـا عَبْـدُك، ظَلَمْـتُ نَفْسـي وَاعْـتَرَفْتُ بِذَنْبـي فَاغْفِرْ لي ذُنوبي جَميعاً إِنَّـه لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إلاّ أَنْت، وَاهْدِنـي لأَحْسَنِ الأَخْلاقِ لا يَهْـدي لأَحْسَـنِها إِلاّ أَنْـت، وَاصْـرِف عَـنّْي سَيِّئَهـا، لا يَصْرِفُ عَـنّْي سَيِّئَهـا إِلاّ أَنْـت، لَبَّـيْكَ وَسَعْـدَيْك، وَالخَـيْرُ كُلُّـهُ بِيَـدَيْـك، وَالشَّرُّ لَيْـسَ إِلَـيْك، أَنا بِكَ وَإِلَيْـك، تَبـارَكْتَ وَتَعـالَيتَ، أَسْتَغْـفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيك
Wajjahtu wajhiya liLLadhiy fatwaras-samaawaati wal ardhwa haniyfan wamaa ana minal mushrikiyn. Inna swalaatiy, wanusuky, wamahyaaya wamamaatiy liLLaahi Rabbil ‘aalamiyn. Laa shariyka Lahu wabidhaalika umirtu wa anaa minal Muslimiyn. Allaahumma Antal-Maliku laa ilaaha illa Anta. Anta Rabbiy wa ana ‘abduka, dhwalamtu nafsiy wa’taraftu bidhambiy faghfirly dhunuwbiy jamiy’an innahu laa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta. Wahdiniy liahsanil-akhlaaqi laa yahdiy liahsanihaa illa Anta, waswrif ‘annyi sayyiahaa laa yaswrif ‘anniy sayyiahaa illa Anta. Labbayka wasa’dayka walkhayru kulluhu biyadika, wash-sharru laysa Ilayka, ana bika wa Ilayka, Tabaarakta wa Ta’aalayta, astaghfiruka wa atuwbu Ilayka
Nimeuelekeza uso wangu kwa yule Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi hali ya kuelemea katika haki, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika Swalaah yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allaah Rabb walimwengu, Hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa nami ni katika Waislamu. Ee Allaah, Wewe Ndiye Mfalme, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe Ndiye Rabb wangu na mimi ni mja Wako. Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nighufurie madhambi yangu yote, hakika haghufurii madhambi, ila Wewe. Na niongoze kwenye husnul-khuluq (tabia njema) kwani haongozi kwenye husnul-khuluq (tabia njema) ila Wewe. Niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wa kuniepusha na tabia mbaya ila Wewe. Naitikia mwito Wako, na nina furaha kukutumikia, na kheri zote ziko mikononi Mwako, na shari haitoki Kwako, mimi nimepatikana kwa ajili Yako, na nitarudi Kwako, Umebarikika na Umetukuka, nakuomba maghfira na narudi Kwako kutubia [Muslim]
Bonyeza Upate Du’aa Kwa Sauti: