19-Hadiyth Husnul-Khuluq: Ubakhili Na Khulqa Mbaya Hazijumuiki Kwa Muumini
Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)
Hadiyth Ya 19
Ubakhili Na Khulqa Mbaya Hazijumuiki Kwa Muumini
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {خَصْلَتَانِ لَا يَجْتَمِعَانِ فِي مُؤْمِنٍ: اَلْبُخْلُ، وَسُوءُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَفِي سَنَدِهِ ضَعْفٌ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mambo mawili hayajumuiki kwa Muumini: ubakhili na khulqa (tabia) mbaya.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na katika isnaad yake kuna udhaifu]