Pudini Ya Mkate, Jibini Na Siagi
Pudini Ya Mkate, Jibini Na Siagi
Vipimo
Slesi za mkate - 8
Jibini ya malai (cream cheese) - 3 Vijiko vya supu
Siagi - Kiasi
Maziwa - 2 vikombe
Maziwa ya kuvukiza (evaporated milk) - 1/4 Kikombe
Mayai - 5
Sukari - 5 vijiko vya supu
Vanilla - 1 kijiko cha supu
Zabibu kavu - kiasi kidogo
Namna ya kutayarisha na kupika
- Paka jibini na siagi ueneze vizuri katika slesi za mkate.
- Funika moja juu ya mwenziwe kisha kata slesi za mkate ziwe vipande vya pembe tatu.
- Zipange kwenye bakuli la kupikia katika oveni.
- Pasha moto maziwa kidogo tu, tia sukari na vanilla.
- Piga mayai katika kibakuli kidogo kisha changanya katika maziwa.
- Mwagia maziwa juu ya slesi za mkate.
- Tupia zabibu, kisha tia katika oveni upike katika moto wa 350º kwa muda wa dakika 45 au zaidi kidogo hadi pudini iwive igeuke rangi.
- Epua na tayari kuliwa.
Vidokezo:
Pudini hii huliwa ikiwa dafu dafu, hivyo inafaa siku za baridi.
Ikiwa huna jibini ya malai unaweza kutia siagi pekee.