09-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: ‘Ilmu Inayonufaisha Inaendelea Kumpatia Thawabu Mtu Baada Ya Kufariki
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 09
‘Ilmu Inayonufaisha Inaendelea Kumpatia Ujira Mtu Baada Ya Kufariki
عَنْ أَبِي هُرَيْرَة (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِذَا مَاتَ ابْنُ آدَم انْقَطَعَ عَمَلُهُ إلاَّ مِنْ ثَلاَث: صَدَقَةٍ جَارِيَةٍ أَوْ عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ)) مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Bin Aadam akifa, ‘amali zake hukatika isipokuwa mambo matatu: Swadaqah inayoendelea, au elimu inayonufaisha, au mtoto mwema anayemuombea du’aa)). [Muslim]