10-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Dunia Imelaaniwa Isipokuwa Matatu Dhikru-Allaah ‘Aalim Na Mwanafunzi
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 10
Dunia Imelaaniwa Isipokuwa Matatu Dhikru-Allaah ‘Aalim Na Mwanafunzi Wa Dini
عن أبي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (( أَلاَ إِنَّ الدُّنْيَا مَلْعُونَةٌ مَلْعُونٌ مَا فِيهَا إِلاَّ ذِكْرُ اللَّهِ ، وَمَا وَالاَهُ ، وَعَالِمٌ أَوْ مُتَعَلِّمٌ)) الترمذي وقال: حَدِيثٌ حَسَنٌ
Imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: ((Zindukeni! Dunia imelaaniwa, kimelaaniwa kilichomo humo isipokuwa kumtaja Allaah na jambo linalokaribiana na hilo (la kumtii Allaah), ‘Aalim na anayejifunza [Dini])) [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan]