15-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Husda Imeruhusika Kwa Aliyejaaliwa ‘Ilmu Akaifanyia Kazi Na Kuifundisha

Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

 

Hadiyth Ya 15

Husda Imeruhusika Kwa Aliyejaaliwa ‘Ilmu Akaifanyia Kazi Na Kuifundisha

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ "‏ لاَ حَسَدَ إِلاَّ فِي اثْنَتَيْنِ رَجُلٌ آتَاهُ اللَّهُ مَالاً فَسَلَّطَهُ عَلَى هَلَكَتِهِ فِي الْحَقِّ، وَرَجُلٌ آتَاهُ اللَّهُ حِكْمَةً فَهْوَ يَقْضِي بِهَا وَيُعَلِّمُهَا ‏"‏‏.‏

 

Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimsikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  "Hakuna husda isipokuwa kwa wawili: Mtu ambaye Allaah amempa mali na anaitumia katika njia sahihi, na mtu ambaye Allaah Amempa hekima (yaani, elimu ya Qur-aan na Sunnah) na anafanya maamuzi yake kufuatana nayo na anawafundisha wengine." [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Faida:

 

Katika lugha ya kiarabu ‘Hasad’ (husuda na wivu) hurejea kwa mtu anayemuonea wivu mwenzake na kuhusudu alichokuwa nacho na kutamani neema ile imuondokee na ije kwake. Jambo hili limekatazwa. Ikiwa mtu anatamani apate kitu fulani lakini hataki vile vile kimuondokee mwenzake, jambo hili linaitwa ‘Hiqd’. Hisia hii inahitajika katika mambo ya kidini.  Kwa hiyo Hadiyth hii imekusudiwa husda ya kutamani mtu awe kama hao watu wa aina mbili, na sio hiqd ambayo inamaanisha kutamani mtu neema za hao watu wawili ziwaondokee.

 

 

 

 

Share