16-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Fadhila Za ‘Aalim Na ‘Ulamaa Ni Warithi Wa Manabii
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 16
Fadhila Za ‘Aalim Na ‘Ulamaa Ni Warithi Wa Manabii
عن أبي الدرداء رضي الله عنه قال : سمعتُ رسولَ الله صلَّى الله عليه وسلَّم يقول: «مَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَطْلُبُ فِيهِ عِلْمًا سَلَكَ اللهُ بِهِ طَرِيقًا مِنْ طُرُقِ الجَنَّةِ، وَإِنَّ المَلَائِكَةَ لَتَضَعُ أَجْنِحَتَهَا رِضًا لِطَالِبِ العِلْمِ، وَإِنَّ العَالِمَ لَيَسْتَغْفِرُ لَهُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَمَنْ فِي الأَرْضِ وَالحِيتَانُ فِي جَوْفِ المَاءِ، وَإِنَّ فَضْلَ العَالِمِ عَلَى العَابِدِ كَفَضْلِ القَمَرِ لَيْلَةَ البَدْرِ عَلَى سَائِرِ الكَوَاكِبِ، وَإِنَّ العُلَمَاءَ وَرَثَةُ الأَنْبِيَاءِ، وَإِنَّ الأَنْبِيَاءَ لَمْ يُوَرِّثُوا دِينَارًا وَلَا دِرْهَمًا، إِنَّمَا وَرَّثُوا العِلْمَ، فَمَنْ أَخَذَهُ أَخَذَ بِحَظٍّ وَافِرٍ» [رواه أبو داود (٣٦٤١)، والترمذي (٢٦٨٢)، وصحَّحه الألباني في «صحيح أبي داود» (٣٦٤١)].
Abu Dardaai (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Mwenye kuifuata njia ya kuitafua ‘Ilmu, Allaah Humfanyia wepesi njia ya Jannah, na hakika ya Malaika wanagubika mbawa zao kwa mwenye kutafuta ‘Ilmu, wapo radhi kwa anayoyafanya, na hakika ‘Aalim (Mwanazuoni) anaombewa maghfira kwa aliyepo katika mbingu na ardhi hata samaki baharini, na fadhila za ‘Aalim juu ya mwenye kufanya ‘ibaadah ni kama fadhila za mwezi juu ya nyota nyengine, na hakika ya ‘Ulamaa ni warithi wa Manabii, na hakika Manabii hawarithishi dinari wala dirham, na hakika (wao) wanarithisha ‘Ilmu. Basi yeyote atakayechukua (‘Ilmu hiyo), amechukua kitu bora.)) [Imepokewa na Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (3641)]