17-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Anayejifunza ‘Ilmu Kwa Ajili Ya Cheo Pekee Hatopata Harufu Ya Jannah
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 17
Anayejifunza ‘Ilmu Ya Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Kwa Ajili Ya Cheo Pekee Hatopata Harufu Ya Jannah
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ تَعَلَّمَ عِلْمًا مِمَّا يُبْتَغَى بِهِ وَجْهُ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ لاَ يَتَعَلَّمُهُ إِلاَّ لِيُصِيبَ بِهِ عَرَضًا مِنَ الدُّنْيَا لَمْ يَجِدْ عَرْفَ الْجَنَّةِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ " . يَعْنِي رِيحَهَا .
Abuu Huraryah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kujifunza ‘Ilmu za Allaah (عَزَّ وَجَلَّ), hajifunzi isipokuwa kupata cheo ndani ya dunia, hatoipata (hata) harufu ya Jannah (Pepo) Siku Ya Qiyaamah.” [Abuu Daawuwd]