15-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kwenda Kwenye Swalaah ya Iyd na Kuwazuru Wagonjwa, Hijja, Jihadi (Vita), Kufuata Jeneza na Mfano Wake Katika Njia Moja na Kurudi Kwa Njia Fursa za 'Ibaadah

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب استحباب الذهاب إِلَى العيد وعيادة المريض والحج والغزو والجنازة ونحوها من طريق ، والرجوع من طريق آخر لتكثير مواضع العبادة

15-Mlango Wa Kupendeza Kwenda Kwenye Swalaah ya Iyd na Kuwazuru Wagonjwa, Hijja, Jihadi (Vita), Kufuata Jeneza na Mfano Wake Katika Njia Moja na Kurudi Kwa Njia Fursa za 'Ibaadah

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن جابر رضي الله عنه ، قَالَ: كَانَ النبي صلى الله عليه وسلم إِذَا كَانَ يومُ عيدٍ خَالَفَ الطَّريقَ . رواه البخاري .

Amesema Jaabir (Radhwiya Allahu 'anhu): "Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) itakapofika siku ya Iyd hubadilisha njia." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عُمَرَ رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يَخْرُجُ مِنْ طَريق الشَّجَرَةِ ، وَيَدْخُلُ مِنْ طَريقِ الْمُعَرَّسِ ، وَإِذَا دَخَلَ مَكَّةَ ، دَخَلَ مِن الثَّنِيَّةِ الْعُلْيَا ، وَيَخْرُجُ مِنَ الثَّنِيَّةِ السُّفْلَى . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatoka mji wa Madiynah kupitia njia ya Shajarah na anaingia kupitia Makkah kutokea Thaniyyatul 'Ulya na akatoka kupitia Thaniyyatus Suflaa (Thaniyyatul ni njia nyembamba baina ya majabali mawili). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share