16-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuanza kwa Upande wa Kulia Katika Kila Lenye Kupendeza Kama Kutawadha, Kuoga, Kutayamam, Kuvaa na Kuingia Msikitini
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب تقديم اليمين في كل مَا هو من باب التكريم
16-Mlango Wa Kuanza kwa Upande wa Kulia Katika Kila Lenye Kupendeza Kama Kutawadha, Kuoga, Kutayamam, Kuvaa na Kuingia Msikitini
كالوضوءِ وَالغُسْلِ وَالتَّيَمُّمِ ، وَلُبْسِ الثَّوْبِ وَالنَّعْلِ وَالخُفِّ وَالسَّرَاوِيلِ وَدُخولِ الْمَسْجِدِ ، وَالسِّوَاكِ ، وَالاكْتِحَالِ ، وَتقليم الأظْفار ، وَقَصِّ الشَّارِبِ ، وَنَتْفِ الإبْطِ ، وَحلقِ الرَّأسِ ، وَالسّلامِ مِنَ الصَّلاَةِ ، وَالأكْلِ ، والشُّربِ ، وَالمُصافحَةِ ، وَاسْتِلاَمِ الحَجَرِ الأَسْوَدِ ، والخروجِ منَ الخلاءِ ، والأخذ والعطاء وغيرِ ذَلِكَ مِمَّا هُوَ في معناه . ويُسْتَحَبُّ تَقديمُ اليسارِ في ضدِ ذَلِكَ ، كالامْتِخَاطِ وَالبُصَاقِ عن اليسار ، ودخولِ الخَلاءِ ، والخروج من المَسْجِدِ ، وخَلْعِ الخُفِّ والنَّعْلِ والسراويلِ والثوبِ ، والاسْتِنْجَاءِ وفِعلِ المُسْتَقْذرَاتِ وأشْبَاه ذَلِكَ .
Pia kupiga msuwaki, kupaka wanja, kukata kucha, kupunguza masharubu, kung'oa nywele za makapwani na kunyoa nywele. Na pia kutoa salamu ya kumaliza Swalaah, kula na kunywa, kupeana mikono, kulibusu Hajaril Aswad (Jiwe jeusi katika Al-Ka'abah) na kutoka chooni, kupokea na kupeana kitu na shughuli nyengine zilizo sawa na hizo. Na inapendeza kutanguliza kushoto katika mambo yaliyo kinyume na hayo kama kutoa makamasi na kutema mate upande wa kushoto, kuingia chooni, kutoka Msikitini, kuvua soksi na viatu, suruali na nguo, kuosha sehemu za siri baada ya kumaliza haja na kufanya kazi chafu na mfano wake...
قَالَ الله تَعَالَى:
فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ﴿١٩﴾
Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake; atasema: Hebu chukueni someni kitabu changu! [Al-Haaqah: 19]
فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿٨﴾
Basi watu wa kuliani; je, ni nani watu wa kuliani?
وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ ﴿٩﴾
Na watu wa kushotoni; je, ni nani watu wa kushotoni? [Al-Waaqi'ah: 8-9]
Hadiyth – 1
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُعْجِبُهُ التَّيَمُّنُ في شَأنِهِ كُلِّهِ : في طُهُورِهِ ، وَتَرَجُّلِهِ ، وَتَنَعُّلِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapenda kuanza kuliani katika mambo yake yote: Katika kijitwahirisha kwake, kuchana nywele zake na kuvaa viatu vyake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَتْ يَدُ رسول الله صلى الله عليه وسلم اليُمْنَى لِطُهُورِهِ وَطَعَامِهِ ، وَكَانَتِ الْيُسْرَى لِخَلائِهِ وَمَا كَانَ مِنْ أذَىً . حديث صحيح ، رواه أَبُو داود وغيره بإسنادٍ صحيحٍ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitumia mkono wake wa kuume kwa kujitwahirisha na kulia chakula. Na alikuwa anautumia mkono wake wa kushoto kujisafisha anapoingia haja (chooni) na mambo mengine kama hayo." [Hadiyth Swahiyh, Abu Daawuwd na wengineo kwa Isnaad iliyo Swahiyh].
Hadiyth – 3
وعن أم عطية رضي الله عنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ لهن في غَسْلِ ابْنَتِهِ زَيْنَبَ رضي الله عنها : (( ابْدَأنَ بِمَيَامِنِهَا ، وَمَوَاضِعِ الوُضُوءِ مِنْهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ummu 'Atwiyyah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwaambia walipokuwa wanamuosha binti yake, Zaynab (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Anzeni kuliani kwake na sehemu za udhu wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا انْتَعَلَ أحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِالْيُمْنَى ، وَإِذَا نَزَعَ فَلْيَبْدأْ بِالشِّمَالِ . لِتَكُنْ اليُمْنَى أوَّلَهُمَا تُنْعَلُ ، وَآخِرُهُمَا تُنْزَعُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mmoja wenu anapovaa viatu aanze kwa mguu wa kulia na anapovua aanze kwa mguu wa kushoto. Hivyo, uwe mguu wa kulia wa mwanzo kuvaa nao viatu na wa mwisho kuvua viatu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن حفصة رضي الله عنها : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يجعل يَمينَهُ لطَعَامِهِ وَشَرَابِهِ وَثِيَابِهِ ، وَيَجْعَلُ يَسَارَهُ لِمَا سِوَى ذَلِكَ . رواه أَبُو داود والترمذي وغيره .
Imepokewa kutoka kwa Hafswah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliujaalia mkono wake wa kulia ni wa kulia chakula, na kunywea kinywaji na kuvulia nguo. Na aliutumia mkono wake wa kushoto kwa mambo mengine yasiyokuwa hayo." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy na wengineo]
Hadiyth – 6
وعن أَبي هُريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا لَبِسْتُمْ ، وَإِذَا تَوَضَّأتُمْ ، فَابْدَأوا بأيَامِنِكُمْ )) حديث صحيح ، رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Ahu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anzeni kwa mkono wenu wa kulia mnapovaa nguo na mnapo tawadha." [Hadiyth Swahiyh, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 7
وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أتى مِنىً ، فَأتَى الْجَمْرَةَ فَرَمَاهَا ، ثُمَّ أتَى مَنْزِلَهُ بِمِنَىً ونحر ، ثُمَّ قَالَ لِلحَلاَّقِ : (( خُذْ )) وأشَارَ إِلَى جَانِبهِ الأَيْمَنِ ، ثُمَّ الأَيْسَرِ ، ثُمَّ جَعَلَ يُعْطِيهِ النَّاسَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية : لما رمَى الجَمْرَةَ ، وَنَحَرَ نُسُكَهُ وَحَلَقَ ، نَاوَلَ الحَلاَّقَ شِقَّهُ الأَيْمَنَ فَحَلَقَهُ ، ثُمَّ دَعَا أَبَا طَلْحَةَ الأنْصَارِيَّ رضي الله عنه ، فَأعْطَاهُ إيَّاهُ ، ثُمَّ نَاوَلَهُ الشِّقَّ الأَيْسَرَ ، فَقَالَ : (( احْلِقْ )) ، فَحَلَقَهُ فَأعْطَاهُ أَبَا طَلْحَةَ ، فَقَالَ : (( اقْسِمْهُ بَيْنَ النَّاسِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifika Mina, akalielekea Jamarah na kutupa vijiwe. Baada ya hapo alirudi kwenye hema lake hapo Mina na kuchinja mnyama wake. Kisha alimwambia kinyozi: "Chukua (yaani amnyoe)." Akamuashiria upande wa kuliani (mwa kichwa chake) na kisha kushoto. Akawa anawapatia nywele zake watu (aliponyolewa). [Al-Bukhaariy, Muslim, abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Na katika riwaayah nyingine: Baada ya kurusha vijiwe kwenye Jamarah na kuchinja mnyama wake na akajitayarisha kunyolewa, alimuonyesha kinyozi upande wa kulia naye akamnyoa. Kisha alimuita abu Twalhah Al-Ansaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) na akampatia hizo nywele. Baada ya hilo, alimuonyehsa kinyozi upande wa kushoto, na akanyolewa upande huo pia. akampatia Abu Twalhah nywele hizo na kumwambia: "Wagawanyie watu."