Imaam Ibn Baaz: Kuswali Gizani Inajuzu?
Kuswali Gizani Inajuzu?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, inajuzu kuswali kwenye giza?
JIBU:
Naam, hakuna ubaya wowote, lau kama mtu ataswali sehemu yenye giza hakuna ubaya wowote, alikuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali kwenye chumba chake ilihali hakuna taa.
[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb (371/7)]
