Biskuti Za Kastadi
Biskuti Za Kastadi
Vipimo
Unga 6 Vikombe
Sukari ya kusaga 2 vikombe
Siagi 500 gm
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Kastadi ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
- Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli.
- Tia unga na baking powder na Kastadi.
- Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray).
- Pika (bake) katika oven moto wa 350° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)