Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani)
Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani)
Vipimo:
Unga - 3 mug za chai
Samli - ½ mug ya chai
Maziwa - 1¼ mug ya chai
Baking powder - 2 vijiko vya chai
Mjazo
Njugu zilizomenywa vipande vipande - 2 vikombe cha chai
Sukari - ½ kikombe cha chai
Iliki - 1 kijiko cha chai
Nazi iliyokunwa - 2 vikombe vya chai
Shira
Sukari - 2 vikombe vya chai
Maji - 1 kikombe cha chai
Ndimu - 1
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1-Changanya unga na samli kisha tia baking powder na maziwa. Ukande ulainike kisha
uwache kama dakika 5 uumuke.
2-Kwenye bakuli nyingine changanya njugu, sukari na iliki.
3-Kata madonge madogo dogo sukuma kila donge duara jembamba, kisha tia kijiko cha mchanganyiko wa njugu juu yake ifunikie juu yake na ibane pembeni kama inavyoonyesha katika picha.
4-Panga kwenye treya isiyoganda (non stick) kisha choma kwenye oven kwa moto wa chini
(bake) 350° C kwa dakika kama 15-20.
5-Chemsha maji na sukari katika sufuria ndogo kisha tia ndimu acha ichemke mpaka inatenate unapoigusa.
6-Kwenye sahani ya chali mimina nazi iliyokunwa.
7-Vibiskuti vikiwa tayari vya motomoto chovea kwenye shira kisha zungushia katika nazi iliyokunwa,
panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
Kidokezo:
Unaweza kutumia tende badala ya njugu.