Biskuti Za Cornflakes
Biskuti Za Cornflake
VIPIMO
Unga - 1 Kikombe
Sukari ya kusaga - 3/4 Kikombe
Siagi - 125 gms
Yai - 1
Baking powder - 1/2 kijiko cha chai
Zabibu kavu - 1/2 kikombe
Cornflakes iliyovunjwa (crushed) - 2 Vikombe
Vanilla - 1 kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.
- Tia baking powder, zabibu na unga na changanya vizuri.
- Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.
- Tengeneza viduara vidogo vidogo.
- Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni.
- Pika katika moto wa 350ºF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.