Vileja Vya Karanga
Vileja Vya Karanga
VIPIMO
Mayai - 5
Sukari - 450gm (1 lb)
Unga wa Ngano - 1 kg
Siagi - 450gm (1 lb)
Baking powder - ½ Kijiko cha chai
Unga wa Custard - Vijiko 2 vya chakula
Karanga za kusaga - 250gm
Jam - ½ kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Chukua bakuli la kiasi, weka sukari na siagi.
- Changanya sukari na siagi kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cakemixer), mpaka sukari ichanganyike na siagi.
- Vunja yai moja moja na weka kiini chake kwenye mchanganyiko wa sukari na siagi, endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri. Hifadhi ute wa mayai ndani ya kibakuli.
- Mimina unga wa ngano ndani ya mchanganyiko wako huku ukichanganya Changanya unga wa custard na baking powder.
- Tengeneza viduara vidogo vidogo.
- Vichovye viduara ndani ya ute wa yai kisha zimwagie unga wa karanga na kuzipanga kwenye tray ya kuchomea.
- Weka dole gumba kati kati ya kila kiduara na uweke jam.
- Washa jiko (oven) 350F na uchome vileja vyako kwa dakika 20.
- Toa vileja vyako vipoe na uviweke ndani ya sahani tayari kwa kuliwa.