Biskuti Za Mtindi/Yoghurt
Biskuti Za Mtindi (Yoghurt)
Vipimo
Chenga za biskuti - 3 gilasi
Mtindi (yogurt) - 1 Kopo (750g)
Maziwa ya unga - 1 gilasi
Siagi - 10 Vijiko vya supu
Sukari - ½ gilasi
Lozi zilizomenywa vipande vipande - ½ gilasi
Nazi iliyokunwa - ½ gilasi
Vanilla - 1 Kijiko cha supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika mashine ya kusagia (blender), tia mtindi, sukari, siagi na vanilla na usage pamoja hadi ichanganyike.
- Mimina katika bakuli la kiasi.
- Tia vitu vilivyobakia na uchanganye vizuri.
- Mimina kwenye treya ya kuchomea na uvumbike katika oveni moto wa 350° hadi ishikamane na kuwa tayari.
- Iaache ipoe kisha katakata vipande na tayari kwa kuliwa.
Kidokezo:
Baada yakuwa imeshaiva, ukipenda unaweza kupakiza jamu au karameli ya tayari kwa juu, kisha ukarudisha kwenye oveni moto wa juu kidogo kwa ladha nzuri zaidi.