Biskuti Za Tangawizi
Biskuti Za Tangawizi
Vipimo
Unga - 2 Vikombe
Cocoa ya unga - 1 Kijiko cha supu
Sukari ya hudhurungi - 1 Kikombe
Siagi - ¾ Kikombe
Yai - 1
Molasses - ¼ Kikombe
Baking soda - 2 vijiko vya chai
Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu
Karafuu ya unga - ½ kijiko cha chai
Chumvi ½ kijiko cha chai
Vanilla ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando.
- Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti.
- Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili.
- Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri.
- Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike.
- Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri.
- Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.)
- Tengeneza viduara vidogo vidogo.
9-Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka
10-Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.
11-Oka katika oven 350ºF kwa muda wa dakika 15.
12-Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi.
13Panga kwenye sahani tayari kuliwa.