Visheti Vya Kukandiwa Siagi Vya Kastadi
Visheti Vya Kukandiwa Siagi Vya Kastadi
Vipimo
Unga - 4 Vikombe vya chai
Siagi - 1 Kikombe cha chai
Kastadi (Custard) vijiko vya supu
Hiliki ½ Kijiko cha chai
Shira:
Sukari - 2 Vikombe vya chai
Maji - 1 Kikombe cha chai
Vanilla ½ Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi, kastadi na hiliki.
- Changanya vizuri isiwe na madonge.
- Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
- Halafu utakatakata vidoge vidogo design upendayo
- Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya brown light, kisha viepue vichuje mafuta. .
- Changanya visheti na shira uchaganye vizuri.
- Vimwage katika sinia vipoe vikiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)