Biskuti Za Ufuta Na Jam
Biskuti Za Ufuta Na Jam
Vipimo
Unga vikombe 2
Sukari ya kusaga 1/4 Kikombe
Siagi 250 gms
Jam kisia
Ufuta kisia
Vanilla 1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai, sukari na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.
- Tia baking powder, na unga na changanya kwa mkono vizuri.
- Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.
- Tengeneza viduara vidogo vidogo.
- Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam, halafu juu yake paka mayai na unynyuzie ufuta.
- Pika katika moto wa chini 350ºF kwa muda wa dakika 20-25.
- Tayari kwa kuliwa.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)