Biskuti Za Jam
Biskuti Za Jam

Vipimo
Unga 2 ½ gilasi
Sukari ¾ gilasi
Samli 1 gilasi
Mayai 2
Baking powder 2 kijiko vya chai
Vanilla 1 ½ kijiko cha chai
Maganda ya chungwa 1
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia kwenye machine ya kusagia (blender) mayai, sukari, vanilla, samli na maganda ya chungwa, saga vizuri.
- Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya.
- Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni.
- Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake.
- Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam.
- Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180 C.
Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)
