Ma’muul Za Lozi (Lebanon)
Ma’muul Za Lozi (Lebanon)
Vipimo:
Siagi - 400 gms
Sukari - 2 vijiko vya supu
Unga - 4 – 5 vikombe
Mayai - 2
Vanilla ½ kijiko cha chai
Lozi - 2 vikombe
Sukari ya unga (icing sugar) - 1 kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika.
- Tia siagi na sukari katika mashine ya keki kisha usage hadi iwe laini kabisa.
- Tia ute wa mayai uchanganye vizuri.
- Tia vanilla
- Tia lozi zilomenywa na kukatwakatwa slaisi (blanched sliced almonds).
- Tia unga kidogo kwanza katika mashine uchanganye vizuri. Kisha zima mashine na uendelee kutia unga kidogo kidogo ukichanganya kwa mkono hadi ushikane.
- Tia katika mbao ya ma’muul (kama kwenye picha) ubonyeze ndani ili itengenezeke duara.
- Vipange katika treya ya kupikia katika oveni.
- Choma (bake) kwa moto mdogo kabisa takriban 300°C .
- Vikiiva vitoe viache vipoe kisha nyunyizia sukari ya unga (icing sugar) na uviweke katika vijikombe vya karatasi.
Kidokezo:
Kiasi cha unga hadi mchanganyiko wa Ma’muul ushikane inategemea saizi ya mayai.