Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe
Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe
Vipimo
Unga wa ngano - 1 Kilo
Siagi - ¼ kilo
Mayai 2
Kastadi (custard) - 3 vijiko vya supu
Baking powder - 1 kijiko cha chai
Maziwa - 1 ½ gilasi
Mafuta Ya kukaangia - kiasi katika karai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka unga katika bakuli kubwa kisha changanya na unga wa kastadi na baking powder.
- Tia siagi uchanganye vizuri.
- Tia mayai, kisha maziwa ya baridi uchanganye vizuri usiukande sana.
- Fanya madonge kisha kata vipande vidogovidogo kisha ubonyeze kwa kidole uvikwaruze kwenye chujio lenye tundu itokee shepu (design) yake.
5- Tia mafuta katika karai yakipata moto, kaanga visheti hadi viive. Usiache hadi vikageuka rangi sana.
6- Eupua, weka katika sufuria au chombo kikubwa kusubiri shira.
Vipimo Vya Shira
Sukari - ½ kilo
Hiliki ilosagwa - 1 kijiko cha chai
‘arki (rose flavor) - 5 matone
Maji - 1 gilasi
Namna Ya Kutyarisha
- Changanya sukari na maji uipike hadi iwe nzito.
- Ukiona mapovu yanatoka tia hilik na ‘arki .
- Mwagia katika visheti uchanganye vizuri hadi vishike na sukari.