Nangatai
Nangatai
Vipimo
Unga wa ngano - 2 - 2 ¼ Vikombe
Siagi - 1 ½ Kikombe
Sukari - 1 Kikombe
Yai - 1
Vanilla -Tone moja
Baking Powder -kijiko 1 cha chai
Chumvi - Kiasi kidogo (pinch)
Unga wa Kastadi - 2 Vijiko vya supu
Namna ya kutayarisha na kupika
- Changanya vitu vyote isipokuwa unga.
- Tia unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko uwe sawa.
- Kisha fanya duara ndogo ndogo uzipange kwenye treya na utie rangi katikati.
- Halafu zichome katika moto wa 300°F kwa muda wa dakika 20 - 25 na zisiwe browni .
- Kisha panga kwenye sahani tayari kuliwa na chai.