Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa (Cocoa Coffee Biscuits)
Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa (Cocoa Coffee Biscuits)
Vipimo
Maji baridi – kikombe 1
Biskuti za kawaida – paketi 2
Kaukau (cocoa) – vijiko 3 vya kulia
Kahawa ya unga – kijiko 1 cha kulia
Njugu mchanganyiko zilokatwakatwa – kikombe 1
Sukari – kiasi upendavyo
- Changanya maji na kaukau na kofi na sukari
- Katakata biskuti kisha tia paketi moja na nusu uchanganye vizuri.
- Kisha nusu ya biskuti zilobakia katakata vipande vikubwa na weka juu ya mchanganyiko, kisha changanya kidogo tu.
- Weka katika foil paper na zungusha (roll)
- Kisha fungua umwagie njugu au mkassaraat zilosagwa
- Kisha roll katika foil paper na uweke katika freezer mpaka igande
- Kisha kata kata slices na iko tayari
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)