029-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AL-MUJIYB
أسماء الله الحسنى وصفاته
Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake
الْمُجِيب
AL-MUJIYB
Al-Mujiyb: Mwenye Kuitikia
Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Ndiye mwenye kujibu maombi ya wenye kuomba, na kupokea ‘Ibaadah za wenye kuomba, Yeye (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Hamkatishi tamaa Muumini kwa du’aa yake wala Harudishi maombi ya Muislaam. Allaah Al-Mujiyb Anaomba aombwe na waja Wake wote katika maombi ya Dini na dunia yao katika chakula, mavazi, makazi kama wanavyoomba hidaaya, maghfirah, islahi na mengineyo. Majibu ya Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) yako aina mbili:
Kwanza: Majibu ya jumla kwa waombaji wote:
Anaitikia maombi ya waja Wake vyovyote walivyo, popote walipo, katika hali yoyote, kama Alivyowaahidi katika ahadi Yake ya kweli ambayo haendi kinyume nayo, Anaposema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ﴿٦٠﴾
Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingika Jahanam wadhalilike. [Ghaafir: 60]
Hilo ni jibu la wote walioomba.
Pili: Majibu maalum:
Wenye kumuomba Allaah Al-Mujiyb na wenye kufuata Shariy’ah Zake, wenye ikhlaasw katika ‘ibaadah na maombi yao Anaposema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ﴿١٨٦﴾
Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu; Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]
Basi waniitikie Mimi
Yaani: Wanitii amri Zangu, na waniombe, na pindi watakaponiomba, nitawajibu.
Naye Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) ni Mwenye kuwajibu majibu maalum kwa wenye haja; Anasema:
أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾
Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea ouvu na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka. [An-Naml: 62]
Na kwa kila aliyekata matarajio Yake katika viumbe Wake na akaelemeza moyo wake kwa Rabb wake, hupata majibu kulingana nayo. Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
يَسْأَلُهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ ﴿٢٩﴾
Wanamuomba Yeye kila aliyekuweko mbinguni na ardhini, kila siku Yeye Yumo katika kujaalia mambo. [Ar-Rahmaan: 29]
Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema katika Hadiyth:
حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ عَمَّارٍ، حَدَّثَنَا الْوَزِيرُ بْنُ صَبِيحٍ، حَدَّثَنَا يُونُسُ بْنُ حَلْبَسٍ، عَنْ أُمِّ الدَّرْدَاءِ، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، عَنِ النَّبِيِّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ فِي قَوْلِهِ تَعَالَى كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ. قَالَ " مِنْ شَأْنِهِ أَنْ يَغْفِرَ ذَنْبًا وَيُفَرِّجَ كَرْبًا وَيَرْفَعَ قَوْمًا وَيَخْفِضَ آخَرِينَ " .
Amesimulia Abu Dardaa kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) amesema kuhusu Kauli ya Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ ﴿٢٩﴾
Kila siku Yeye Yumo katika kujaalia mambo. [Ar-Rahmaan: 29]
“Kwa shani Yake Anaghufuria madhambi, na Anafariji dhiki, na Anawanyanyua watu na kuwaakuwaangusha wengine.” [Ibn Maajah Kitaab Al-Muqaddimah]
Humnyanyua aliyevunjika, humtajirisha tajiri, na hushiba mwenye njaa na humvisha aliye uchi na humponya mgonjwa, na humnusuru mdhulumiwa na humvunja Jabari. Wote humuomba Yeye Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) juu ya kuwa wametofautiana, Naye Hawarudishi katika muradi wao Naye ni mwenye kuwatosheleza.