02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kutokitia Kasoro Chakula na Kupendeza Kukisifu
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب لا يَعيبُ الطّعام واستحباب مَدحه
02-Mlango Wa Kutokitia Kasoro Chakula na Kupendeza Kukisifu
Hadiyth – 1
وعن أَبي هُريرة رضي الله عنه ، قَالَ : مَا عَابَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم طَعَامَاً قَطُّ ، إن اشْتَهَاهُ أكَلَهُ ، وَإنْ كَرِهَهُ تَرَكَهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakukitia kasoro chakula kabisa, akikipenda atakila, na kama hakipendi atakiacha." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah].
Hadiyth – 2
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم سَأَلَ أهْلَهُ الأُدْمَ ، فقالوا : مَا عِنْدَنَا إِلاَّ خَلٌّ ، فَدَعَا بِهِ ، فَجَعَلَ يَأكُلُ ، ويقول : (( نِعْمَ الأُدْمُ الخَلُّ ، نِعْمَ الأُدْمُ الخَلُّ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwauliza watu wa nyumbani kwake wampe mchuzi. Wakasema: "Sisi hatuna chochote isipokuwa siki. Aliwaambia wamletee (hiyo siki). Akawa anaila na kusema: "Mchuzi ulio bora ni siki; Mchuzi ulio bora ni siki." [Muslim]