03-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Anachosema Anayeletewa Chakula Naye Amefunga
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقوله من حضر الطعام وهو صائم إِذَا لَمْ يفطر
03-Mlango Wa Anachosema Anayeletewa Chakula Naye Amefunga
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا دُعِيَ أحَدُكُمْ فَلْيُجِبْ، فَإنْ كَانَ صَائِماً فَلْيُصَلِّ، وَإنْ كَانَ مُفْطِراً فَلْيَطْعَمْ )) رواه مسلم.
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapoalikwa mmoja wenu chakula basi anatakiwa aitikie kwa kukubali mwaliko. Ikiwa amefunga basi aache na ikiwa hakufunga basi ale chakula hicho (kilichoandaliwa)." [Muslim]