05-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kula Kilicho Mbele Yake na Kumpa Waadhi na Kumfundisha Adabu Mwenye Kukosea Katika Kula

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الأكل مِمَّا يليه ووعظه وتأديبه من يسيء أكله

05-Mlango Wa Kula Kilicho Mbele Yake na Kumpa Waadhi na Kumfundisha Adabu Mwenye Kukosea Katika Kula

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن عمر بن أَبي سَلمَة رضي الله عنهما ، قَالَ : كُنْتُ غُلاماً في حِجْرِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، وَكَانَتْ يَدِي تَطِيشُ في الصَّحْفَةِ ، فَقَالَ لي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  يَا غُلامُ ، سَمِّ اللهَ تَعَالَى ، وَكُلْ بِيَمينِكَ ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Abu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Nilikuwa kijana mdogo katika malezi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), mkono wangu ukawa unatembea katika sahani ya chakula. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: "Ee kijana! Mtaje Allaah, na kula kwa mkono wa kuume (kulia) na kula kilicho mbele yako." [Al-Bukhaariy, Musli, Maalik, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 2

وعن سلمةَ بن الأَكْوَع رضي الله عنه : أنَّ رَجُلاً أَكَلَ عِنْدَ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم بِشِمَالِهِ ، فَقَالَ : ((  كُلْ بِيَمِينِكَ )) قَالَ : لا أسْتَطِيعُ . قَالَ : ((  لاَ اسْتَطَعْتَ )) ! مَا مَنَعَهُ إِلاَّ الكِبْرُ ! فَمَا رَفَعَهَا إِلَى فِيهِ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Salamah bin 'Amru bin Al-Akwa' (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Kuna mtu ambaye alikula mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mkono wa kushoto. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 'Kula kwa mkono wa kulia.' Akasema: 'Siwezi.' Akasema: 'Hutaweza.' Haikumfanya yeye asifuate agizo la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa ni kibri, hivyo hakuweza tena kuunyanyua mkono mdomoni mwake." [Muslim]

 

 

 

Share