06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Unaokataza Kubana Tende Mbili na Mfano Wake Katika Tonge Moja Kama Anakula na Wenzake Isipokuwa Kwa Ruhusa Yao
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النّهي عن القِرَانِ بين تمرتين ونحوهما إِذَا أكل جماعة إِلاَّ بإذن رفقته
06-Mlango Wa Unaokataza Kubana Tende Mbili na Mfano Wake Katika Tonge Moja Kama Anakula na Wenzake Isipokuwa Kwa Ruhusa Yao
عن جَبَلَة بن سُحَيْم ، قَالَ : أصَابَنَا عَامُ سَنَةٍ مَعَ ابن الزُّبَيْرِ ؛ فَرُزِقْنَا تَمْراً، وَكَانَ عبدُ الله بن عمر رضي الله عنهما يَمُرُّ بنا ونحن نَأكُلُ، فَيقُولُ : لاَ تُقَارِنُوا ، فإنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَى عنِ القِرَانِ ، ثُمَّ يَقُولُ : إِلاَّ أنْ يَسْتَأذِنَ الرَّجُلُ أخَاهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Jabalah bin Suhaym kwamba: Tulipatikana na ukame mwaka mmoja tukiwa pamoja na Ibn Zubayr, naye akawa anatupa tende na Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) alikuwa anatupitia tukiwa tunakula na kusema: "Musibane tende, hakika Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kubana, kula tende mbili kwa mlo mmoja." Kisha akasema: "Isipokuwa mtu miongoni mwenu atakapomuomba ruhusa ndugu yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]