07-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Anachosema na Anachofanya Mwenye Kula Lakini Asishibe
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقوله ويفعله من يأكل وَلاَ يشبع
07-Mlango Wa Anachosema na Anachofanya Mwenye Kula Lakini Asishibe
عن وَحْشِيِّ بن حرب رضي الله عنه : أنَّ أصحابَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، قالوا : يَا رسولَ اللهِ ، إنَّا نَأكُلُ وَلاَ نَشْبَعُ ؟ قَالَ : (( فَلَعَلَّكُمْ تَفْتَرِقُونَ )) قالوا : نَعَمْ . قَالَ: (( فَاجْتَمِعُوا عَلَى طَعَامِكُمْ، وَاذْكُرُوا اسْمَ اللهِ ، يُبَارَكْ لَكُمْ فِيهِ )) رواه أَبُو داود.
Imepokewa kutoka kwa Wahshiy bin Harb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Sisi tunakula lakini hatushibi." Akasema: "Huenda nyinyi mnakula mbali mbali (kila mtu kivyake)." Wakasema: "Ndio." Akasema: "Kusanyikeni pamoja kwenye chakula chenu (kuleni pamoja) na mtaje jina la Allaah, nanyimtabarikiwa kwayo." [Abu Daawuwd]