Imaam Shurayh Al-Qaadhwiy: Ninapopatwa Msiba Humshukuru Allaah Kwa Mambo Manne
Ninapopatwa Msiba Humshukuru Allaah Kwa Mambo Manne
Imaam Shurayh Al-Qaadhwiy (Rahimahu Allaah)
Amesema Imaam Shurayh Al-Qaadhwiy (Rahimahu Allaah)
“Ninapopatwa na msiba ninamhimidi Allaah kwa mambo manne:
1.Nashukuru kama ikiwa hakuna kubwa zaidi ya hilo
2.Nashukuru nikiruzukiwa subira juu yake
3. Nashukuru ikiwa Allaah Ataniwezesha kutaja neno la Al-Istirjaa nikitaraji thawabu kwa Allaah
4.Na ninashukuru ikiwa msiba haujaweza kuharibu dini yangu."
[Siyar A’laam An-Nubalaa: (7/112)]
Al-Istirjaa ni kusema unapopatwa msiba wowote:
إِنّا للهِ وَإِنَا إِلَـيْهِ رَاجِعُـونَ
Innaa liLLaahi wa innaa Ilayhi raaji’uwn,
Hakika sisi wa Allaah, na hakika sisi Kwake wenye kurejea.
