14-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Karaha ya Kupulizia Ndani ya Kinywaji
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة النفخ في الشراب
14-Mlango Wa Karaha ya Kupulizia Ndani ya Kinywaji
Hadiyth – 1
عن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَى عَن النَّفْخ في الشَّرَاب ، فَقَالَ رَجُلٌ : القَذَاةُ أراها في الإناءِ ؟ فَقَالَ : (( أهرقها )) . قَالَ : إنِّي لا أرْوَى مِنْ نَفَسٍ وَاحدٍ ؟ قَالَ : (( فَأَبِنِ القَدَحَ إِذَاً عَنْ فِيكَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kupulizia ndani ya kinywaji. Akasema mtu mmoja: "Je, nitafanyaje kuhusu vitu vinavyoelea katika kinywaji?" Akasema: "Vitoe." Akasema: "Kiu yangu haimaliziki kwa mkupuo mmoja." Akasema: "Unaweza kupumua, lakini kiweke chombo nje ya mdomo wako." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 2
وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم نهى أن يُتَنَفَّسَ في الإناءِ أَوْ يُنْفَخَ فِيهِ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kupumulia ndani ya chombo na kupulizia ndani yake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]