15-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kubainisha Kujuzu Kunywa Kwa Kusimama na Kubainisha Kuwa ni Bora Zaidi Kunywa Kwa Kukaa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب بيان جواز الشرب قائماً وبيان أنَّ الأكمل والأفضل الشرب قاعداً
15-Mlango Wa Kubainisha Kujuzu Kunywa Kwa Kusimama na Kubainisha Kuwa ni Bora Zaidi Kunywa Kwa Kukaa
Hadiyth – 1
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : سَقَيْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم مِنْ زَمْزَمَ ، فَشَربَ وَهُوَ قَائِمٌ . متفق عَلَيْهِ .
Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilimpa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) maji ya Zamzam akanywa huku amesimama." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]
Hadiyth – 2
وعن النَّزَّالِ بن سَبْرَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : أَتَى عَلِيٌّ رضي الله عنه بَابَ الرَّحْبَةِ ، فَشَربَ قائِماً ، وقال : إنِّي رَأَيْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَعَلَ كما رَأَيْتُمُوني فَعَلْتُ . رواه البخاري .
An-Nazzaal bin Sabrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alikuja 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwenye mlango wa Rahbah (sehemu pana iliyopo kufah) na akanywa akiwa amesimama, na akasema: "Hakika mimi nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya kama mnavyoniona nikifanya." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كُنَّا عَلَى عهدِ رسول الله صلى الله عليه وسلم نَأكُلُ وَنَحْنُ نمشِي ، وَنَشْرَبُ ونَحْنُ قِيامٌ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Tulikuwa tukila katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nasi tunatembea na tukinywa nasi tumesimama." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 4
وعن عمرو بن شعيب ، عن أبيه ، عن جَدِّهِ رضي الله عنه ، قَالَ : رأيتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَشْرَبُ قَائِماً وقَاعِداً . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Amruw bin Shu'ayb kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akinywa kwa kusimama na kwa kukaa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 5
وعن أنس رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم : أنه نَهى أن يَشْرَبَ الرَّجُلُ قَائِماً . قَالَ قتادة : فَقُلْنَا لأَنَسٍ : فالأَكْلُ ؟ قَالَ : ذَلِكَ أَشَرُّ – أَوْ أخْبَثُ – رواه مسلم . وفي رواية لَهُ : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم زَجَرَ عَن الشُّرْب قائِماً .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza kunywa kwa kusimama. Amesema Qataadah: Tukamuuliza Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Je, kula?" Akasema: "Hiyo ni baya zaidi au ni chafu zaidi." [Muslim]
Na katika riwaayah yake nyengine: "Hakika Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekemea kunywa kwa kusimama."
Hadiyth – 6
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يَشْرَبَنَّ أحَدٌ مِنْكُمْ قَائِماً ، فَمَنْ نَسِيَ فَلْيَسْتَقِيء )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asinywe mmoja wenu kwa kusimama, na anayesahau basi ajitapishe." [Muslim]